Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillius
Wambura ameunda tume ya kuchunguza tukio la kifo cha kijana Mandela Petro katika
Mji wa Malampaka Wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu.
Kifo cha kijana huyo kinadaiwa kusababishwa na
Askari wa kituo cha Polisi Malampaka, baada ya kumshambulia kwa vipigo wakimtuhumu
kuiba Baiskeli.
Taarifa iliyotolewa Asubuhi ya leo kwa waandishi
wa Habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe imeeleza kuwa IGP
Wambura ameunda tume hiyo leo ikiwa na watu watano.
Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza tume hiyo
itafanya uchunguzi wa tukio hilo kwa muda gani.
Tukio la kuuawa kwa kijana huyo lilianza kusambaa
katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, ambapo Askari hao wanaotumiwa
wanadaiwa kutoa kiasi cha 200,000 (laki mbili) kama rambirambi kwenye mazishi
ya marehemu.
Ilielezwa kuwa ndugu wa marehemu walipofuatilia
taarifa za chanzo cha kifo cha ndugu yao katika kituo cha Polisi Malampaka,
walielezwa kuwa Askari walimuokoa wakati akishambuliwa na wananchi baada ya
kufumaniwa.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment