Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini [RITA] imesajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa papo hapo kwenye Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya saba saba iliyofanyika tarehe 07/07/2023 kwenye viwanja vya J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akiwakabidhi vyeti vyao vya kuzaliwa wananchi waliojitokeza kujisajili kwenye sikukuu hiiyo ya saba saba, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie amesema kuwa RITA imejipanga vizuri kuwapatia huduma Wananchi kiurahisi na kuwataka kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi kupatiwa huduma kwenye maonesho hayo.
"Nawasihi wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya ya saba saba ,maana tunasajili na kutoa vyeti hapa hapa uwanjani, yaani unajiandikisha leo na cheti unapata leo",amesema.
Aidha baadhi ya wananchi waliojitokeza kusajiliwa na kufanikiwa kupata cheti kwenye viwanja hivyo vya saba saba ambapo maonesho ya 47 ya maonesho ya biashara yanaendelea wameipongeza RITA kwa kuwarahisishia huduma kwa kuwapatia cheti siku hiyo hiyo!!!
"Hawa RITA wako vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa hapa hapa sio mchezo,kwa watu tulivyojaa sikutegemea kupata cheti leo,"amesema Salma Ubuguyu mmoja wa wananchi waliojitokeza kupatiwa cheti cha kuzaliwa.
Post a Comment