MNEC Gungu akabidhi Kanuni za CCM kwa Makatibu Kata.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (MNEC) Gungu Silanga (kulia) akikabidhi vitabu vya Kanuni za CCM kwa ajili ya Makatibu kata mbele ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed.
 

Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.

 

MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa (MNEC), kutoka  Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga amekabidhi vitabu vya kanuni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Makatibu Kata wa mkoa huo ili waendelee kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na kusimamia maadili ya Chama.

 

Aidha Gungu amewataka wanaCCM kuendelea kushikamana wakati huu wanaoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzo mkuu 2025.

 

Gungu aliyasema hayo jana kwenye Maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika kata ya Nyaluhande wilayani Busega Mkoani Simiyu ambapo alisema vitabu hivyo ni moja ya ahadi alizokuwa ameahidi kwa Makatibu hao.

 

‘’Niliahidi kutoa vitabu vya kanuni za CCM kwa Makatibu Kata, leo natimiza ahadi hiyo kwa kutoa vitabu 15 kwa Makatibu kata ya Busega kwa niaba ya wengine…hivyo nawaomba mkafanye kazi kwa kuzingatia miongozi na taratibu zilizomo kwenye kanuni, na Makatibu wengine watavichukua kwa Katibu wa CCM wa Mkoa’’ alisema Gungu.

 

Aidha Gungu aliwataka wanaCCM kutambua juhudi za Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea kuchapa kazi za kuwatumikia Watanzania ambapo ametekeleza ahadi mbalimbali ikiwemo kuboresha huduma za Afya, Elimu, Maji na Umeme.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed alisema Chama Cha Mapinduzi kimefanya mambo makubwa katika nchi hii ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma kijamii.

 

Aliwataka wanaCCM kuendelea kuunga mkono juhudi za Dk. Samia Suluhu Hassan huku akiwata Mabalozi kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba ili CCM ishinde katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

 

Kwenye Maadhimisho hayo CCM ilipokea wanachama wapya 50 waliopatiwa kadi za CCM pamoja na vijana wengine 50 waliopatiwa kadi za Umoja wa Vijana (UVCCM).

 

Aidha, Katika Maadhimisho hayo, Mwenyekiti Shemsa alichangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Nyaruhande, pia aliendesha harambee ambayo alifanikiwa kupata jumla ya mifuko 75 ya saruji na fedha kiasi cha shilingi 850,00/=.

 

MWISHO. 


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akisalimiana na mmoja wa wanaCCM kutoka kata ya Nyaruhande wilayani Busega alipohudhuria sherehe za miaka 47 ya CCM.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (kushoto) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (kulia), katika kati ni Mzee maarufu kutoka kata ya Nyaruhande.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (kushoto) akikabidhi vitabu vya kanuni kwa Katibu CCM wilaya ya Busega Steven Koyo (kulia), vitabu ambavy vilitolewa na MNEC Gungu Silanga (hayupo pichani).
 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (kulia) akiwa ameshika kitabu cha kanuni za CCM mara baada ya kukabidhiwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (MNEC), Gungu Silanga (kushoto).
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akipanda mti kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika jana kata ya Nyaruhande wilayani Busega Mkoani humo.
 
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akikabidhi kadi za Uanachama kwa wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM) waliojiunga katika kata ya Nyaruhande wilayani Busega.
 
 
Wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM) kata ya Nyaruhande wilayani Busega.


Vijana wa Green Guard wakimvisha skafu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed wakati akiwasili kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya CCm yaliyofanyika kata ya Nyaruhande wilayani Busega.


 




Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post