Waandishi wa Habari wafukuzwa kwenye kikao mbele ya Naibu Waziri Habari.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akiongoza kikao cha ushauri cha wilaya (katikati) akiwa pamoja na viongozi wa Halmashauri ya wilaya na Mji wa Bariadi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bariadi na Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Mhandisi Kundo Mathew.

 


Na Mwandishi wetu.

 

Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu wamefukuzwa kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya ya Bariadi (DCC) na Mkuu wa wilaya hiyo Simon Simalenga mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Mhandisi Andrea Kundo, huku ajenda kubwa ikiwa ni kujadili mgawanyo wa Jimbo la Bariadi.

 

Wakati kitoa kauli ya kuwafukuza wanahabari hao, Simalenga amesema ‘’Mmekuja kufanya nini hapa, niliwaambia msiwaalike waandishi wa Habari, nani aliwaalika tena? Waandishi wa Habari tokeni nje na milango ifungwe’’

 

Licha ya waandishi wa habari kualikwa kupitia mwaliko rasmi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kujiandikisha katika daftari la mahudhurio kama ilivyo muongozo unaotolewa na waandaaji wa vikao vya Halmashauri (CC).

 

Licha ya waandishi wa habari kufukuzwa, pia wananchi wengine walifukuzwa kwenye kikao hicho licha ya kuwa wasikilizaji kwa ajili ya kujua maendeleo ya wilaya yao.

 

‘’Ni kuminya uhuru wa vyombo vya habari, kama hatukutakiwa angetuambia kwa utaratibu kupitia aliyetualika na sio kutufukuza bila uungwana kama alivyofanya yeye ni mwandishi wa habari sawa lakini haina maana kuwa yupo juu ya vyombo vya habari na anaweza kupanga nini waandike na nini wasiandike, ajenda ya kugawa jimbo la bariadi ni taarifa ambayo kila mmoja au kila mwanachi anatamani kuelewa kinachoendelea kuhusu jimbo lao ’’ amesema mmoja wa wanahabari.

 

Hadi sasa kikao kinaendelea huku waandishi wa habari wakibakia nje ili kumsubiri Naibu Waziri wa Habari, Teknolijia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ili kupata kauli na maoni yake juu ya kitendo kilichofanywa na Mkuu wa wilaya mbele yake.

 

Mwisho.

 

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.



Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post