Osuri Kosuri mwenyekiti tena wa SIFA.

Viongozi wapya wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Simiyu (SIFA) waliochaguliwa jana wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho. (Katikati) ni Menyekiti wa SIFA Osuri Kosuri ambaye ametetea kiti chake.
 



Na Derick Milton, Simiyu.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Simiyu (SIFA), wamemchagua kwa mara ya pili mfululuzo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Osuri Kosuri, kukiongoza tena chama hicho kwa miaka minne.


Katika uchaguzi uliofanyika leo Mjini Bariadi, Wajumbe hao wamemchangua Kosuri kwa kura zote za ndiyo, ambapo katika nafasi hiyo hakuwa na mpinzani kutokana na kugombea peke yake.


Mara baada ya uchaguzi huo, Kosuri amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama hicho kwa kuendelea kumwani, ambapo ameeleza yeye pamoja na kamati yake tendaji mpya wataendeleza pale ambapo wameishia.


Amesema kuwa kama mwenyekiti ataendelea kuboresha eneo la waamuzi kwenye mkoa huo, lakini pia eneo la soka la watoto kwa lengo kuendelea kuibua vipaji na kuweza kupata timu zinazoweza kushiriki ligi daraja la kwanza, pili na ligi kuu.


“ Nawashukuru sana wajumbe kwa kuendelea kuniamini, kama chama tutaendelea kushirikiana na wadau wa mpira kwenye mkoa wetu hasa serikali kama wadau wakubwa katika kuhakikisha mpira unakua,” alisema Kosuri.


Katika uchaguzi huo wajumbe hao wamempitisha bila kupingwa Kajanja Magesa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu TFF, Rehema Shalali kuwa mwenyekiti chama cha mpira wa miguu wanawake, huku Shedrack Daudi akiteuliwa na Mwenyekiti kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post