SERIKALI KUUTANGAZA MKOA WA SIMIYU KWA WAWEKEZAJI.





Na Mwandishi wetu, Simiyu.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara  inaangalia namna nzuri  ya kuutangaza  mkoa wa simiyu katika sekta ya  Viwanda, Biashara na uwekezaji  kutokana na mkoa huo kuwa na fursa nyingi za kiuchumi.


Naibu Waziri Kigahe ameyasema hayo leo 22 Februari,2025 mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi  ya siku mbili kwa lengo la kutembelea viwanda na akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa huo.


Kigahe  amesema Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi za uwekezaji na kwamba unapaswa kupiga hatua kubwa kimaendeleo .


Naibu Waziri ametembelea kiwanda  cha kuchakata mafuta ya alizeti na mafuta ya kula ya pamba cha mwekezaji wa ndani bugali kilichoko mtaa wa Bundilya halmashauri ya mji wa Bariadi na kiwanda cha kuchambua pamba cha alliance cha mwekezaji wa kigeni kilichoko kasoli wilaya ya Bariadi.



Mwisho.









Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post