WATATU WAFARIKI KWA AJALI MBEYA, YUMO MWANAHABARI.


Na MWANDISHI WETU, Mbeya.

WATU  watatu akiwemo Mwandishi wa habari  Mkoa wa Mbeya Furaha Simchimba, wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea mkoani humo ikihusisha basi kampuni ya CRN na gari la serikali STM.

Ajali hiyo imetokea  Februari 25 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya wakati basi lenye namba T 599 DZQ likilipita gari la serikali lenye namba 6167 bila kuchukua tahadhari na kugongana nje ya barabara na kusababisha vifo hivyo na majeruhi saba akiwemo mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Mbeya, Epimacus Apolinary, Mwenyekiti na katibu wa UWT mkoa wa Mbeya.

Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) Nebart  Msokwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema kuwa katika ajali hiyo waandishi   waliopata ajali ni Furaha Simchimba, Epimacus Kalokola, na Selemani Ndelage.

Kuwa kwa bahati mbaya  Furaha Simchimba amefariki katika ajali hiyo.

"Wenzetu Kalokola na Selemani wanaendelea na matibabu. Tunaendelea kufanya juhudi za kuwahamisha kutoka Hospital ya Wilaya (Inyala) kuwaleta Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya"

Watu watatu wamefariki dunia akiwemo mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Mbeya Furaha Simchimba na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea mkoani humo ikihusisha basi kampuni ya CRN na gari la serikali STM.

Ajali hiyo imetokea leo Februari 25 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya wakati basi lenye namba T 599 DZQ likilipita gari la serikali lenye namba 6167 bila kuchukua tahadhari na kugongana nje ya barabara na kusababisha vifo hivyo na majeruhi saba akiwemo mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Mbeya, Epimacus Apolinary, Mwenyekiti na katibu wa UWT mkoa wa Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha ajali hiyo akieleza kuwa kati ya majeruhi saba wawili kati yao wapo mahututi.

Simiyu press club inaungana na wanahabari kote nchini kutoa pole nyingi kwa wanahabari mkoa wa Mbeya ,familia na wote walioguswa na msiba huu pia tunawaombea Afya Njema majeruhi wote wa ajali .


Mwisho 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post