ENG. KUNDO AHITIMISHA UWASILISHAJI WA ILANI KATA ZA NYANGOKOLWA NA NYAKABINDI.

 


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akiongea kwenye Mkutano wa hadhara wa kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 uliofanyika kata ya Nyakabindi, kutoka kulia ni aliyekuwa Diwani wa Kata hito, David Masanja.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amehitisha zoezi la Kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata za Nyangokolwa na Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Uwasilishaji huo unafanya kuzifikia kata 31 za Jimbo la Bariadi huku akiwapongeza Madiwani, viongozi wa CCM na Wananchi kwa kumpa ushirikiano katika uongozi wake wa miaka mitano (2020/2025).


Akizungumza leo kwenye Mkutano wa Hadhara wa kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani, Mhandisi Kundo ameipongeza serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.


"Tunashukuru serikali ya Rais Dkt. Samia kwa fedha nyingi za miradi ya Maendeleo...Kata ya Nyangokolwa mwaka 2015/2020 ilipokea shilingi Mil. 479.67 lakini kwa 2020/2025 imepokea shilingi Bil.4.811 na kata ya Nyakabindi mwaka  2015/2020 ilipokea chini ya shilingi Mil.800,  lakini 2020/2025 imepokea zaidi ya shilingi Bil 4" amesema.


Katika kata ya Nyangokolwa yenye Mitaa 13, Mbunge huyo amekabidhi Mipira 55 ambapo kila mtaa utapata mipira 4 na pea moja ya jezi huku kata hiyo ikikabidhiwa mipira mitatu na jezi pea 1.


Naye kata ya Nyakabindi yenye mitaa 13 imekabidhiwa mipira 55 ambapo kila mtaa utapata mipira 4 na pea moja ya jezi huku kata hiyo ikikabidhiwa mipira mitatu na jezi pea 1.


Mwisho.









Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post