WAKULIMA WA PAMBA MIKOA 17 WAANZA KUUZA PAMBA HUKU BEI IKIPANDA.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


WAKULIMA wa Pamba maeneo mbalimbali kutoka mikoa 17 inayoliza zao la Pamba nchini, wameanza kuuza Pamba yao kupitia vyama vya Msingi "Amcos" katika msimu wa ununuzi wa 20225/2026.


Bei ya Pamba iliyotangazwa na serikali katika msimu wa ununuzi wa 2025/2026 ni shilingi 1,150 baada ya makubaliano ya wawakilishi wa wakulima na Wanunuzi. 


Kutokana na mazingira ya ushindani yaliyowekwa na serikali hadi sasa bei ya ununuzi wa Pamba ya mkulima imefikia 1,200 kwa kilo moja ya Pamba mbegu. 


Aidha, Matumizi ya mizani ya kidigitali yanaendelea kushamiri na kwamba kila mkulima akipima Uzito wa Pamba yake anapewa risti ya kielektroniki inayojumuisha na ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwenye simu yake.



Mwisho.






Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post