Moja ya kizimba cha samaki kilicho ziwa Victoria ambacho kinamilikiwa na kikundi cha Uviusa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu.Na Samwel Mwanga, Busega
JUMLA ya Sh milioni 60 zimetumika kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki katika vizimba utakaowanufaisha kikundi cha vijana cha Uviusa kilichopo kijiji cha Nyamikoma katika wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu.
Katibu wa kikundi cha vijana cha Uviusa, Paul Mchanga leo Agosti 14,2025 akisoma taarifa ya maendeleo ya kikundi hicho kwa Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2025,Ismail Ussi amesema kuwa wameweza kujiajiri.
Amesema kuwa walikopeshwa kiasi hicho cha fedha na serikali na kwa sasa wameanzisha vizimba viwili vya kufugia samaki katika ziwa Victoria eneo la kijiji cha Chumve ambapo kizimba cha kwanza kina samaki wapatao 20,000 na kizimba ncha pili kina samaki wapatao 25,000.
“Tulipata mkopo wa Sh 60 milioni kupitia halmashauri yetu ya Busega ile iliyokuwa inatolewa kwa makundi maalum ya vijana,wanawake na wenye ulemavu na lengo letu kubwa ni kujiajiri,”
“Mradi huu umetoa hadi sasa ajira kwa vijana na kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana,”amesema.
Amesema kuwa mradi umeongeza ujuzi na maarifa kwa kutoa elimu na mbinu bora za kisasa za ufugaji wa samaki.
Mradi huu ulianza kutekelezwa Juni 3,2022 ukiwa na vijana watano ambapo matarajio ya baada ya mavuno ni kilo 12,000 kwa mwaka ambapo wakiuza kwa kila kilo moja sh 7000 watapata Sh 84 milioni na kufanya kuwa na faida ya Sh 24 milioni.
‘Soko la samaki la samaki aina ya sato hawa tunaowafuga ni la uhakika maana uhitaji ni mkubwa na inakadiriwa mauzo ya samaki wote yatafanyika kwa siku moja au mbili.Na samaki hao tutawauza hapa hapa eneo la mradi hatutakuwa na gharama ya usafiri hivyo tunategemea kupata faida kama tulivyoeleza hapo awali,”amesema.
Kiongozi wa Mbio Mwenge wa Uhuru Kitaifa, ameipongeza Halmashauri hiyo ya wilaya ya Busega kwa kutumia mapato yake ya ndani ya asilimia 10 ya kutekeleza agizo la serikali la kutoa mikopo kwa makundi maalum.
"Nikupongeze Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Busega pamoja na Mkuu wa wilaya kwa kuhakikisha maagizo ya serikali ya kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi ya vijana,wanawake na walemavu,”
“Leo hii tumeona vijana wameweka vizimba vyao ndani ya ziwa Victoria hapa tayari wameshajiajiri na wamepambana na tatizo la ajira kwa vijana na niwaombe vijana wengine waige mfano huu na siyo kuallamika kuwa serikali haijawapatia ajira,”amesema.
Mwenge umemaliza mbio zake katika mkoa wa Simiyu,ukiwa wilayani Busega umeweza kutembelea, kuona, kukagua na kuweka mawe katika miradi saba.
Miradi hiyo ni pamoja na daraja la Lutubiga -Mwasamba, Wodi ya wazazi kituo cha Afya Lukungu, Bweni la wasichana shule ya Sekondari Nassa na matumizi ya nishati safi ya kupikia katika shule ya Sekondari Mkula na miradi yote inathamani ya Sh biliomi 1.4
MWISHO.
Wakimbiza Mwenge Kitaifa mwaka 2025 na baadhi ya viongozi wa serikali wa wilaya ya Busega wakiwa kwenye mitimbwi katika ziwa Victoria kwenda kuangalia mradi wa ufugaji wa samaki vizimba katika wilaya ya Busega.
Kingozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi (mwenye miwani) akiwa kwenye mtumbwi akielekea kuangalia mradi wa ufugaji samaki wa kikundi cha Uviusa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu.Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment