Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwanamke
anayefahamika kwa jina la Scholastica Peter mwenye umri wa Miaka 28
mkazi wa mtaa wa Bugwandege kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga,
amewajeruhi watoto wake wawili kwa kuwachoma moto mikononi kwa kile alichodai
alikuwa akiwaonya baada ya kukomba mboga.
Akizungumza
na Mama huyo ambaye amekiri kuwachoma moto watoto hao,
akisema alifanya hivyo kama hatua ya kuwaonya, kwa sababu
wana tabia ya udokozi wa mboga
“Hawa watoto wanatabia ya udokozi ile siku nilipika
mboga tukala usiku tukaibakiza asubuhi nikatoka nikaenda kutembeze mboga
nikakuta wameikomba mboga yote ilikuwa ni mboga ya dagaa nilichanganya na
nyanya ntole”…..
“ Nilikuwa
nawakanya hawasikii hiyo siku nilishikwa na hasira mara ya kwanza niliwapiga ya
pili hii mara ya tatu kulikuwepo jiko lilikuwa na moto na kulikuwepo na jiko
ambalo nilikuwaga natolea mkaa baada ya kuwapiga nikasogeza hilo jiko ndiyo
nikawa nawababua na kijiko”.amesema Scholastica
Akizungumzia
tukio hilo mtendaji wa kata ya Ibinzamata Victor Kajuna amesema
kuwa taarifa hizo amezipata leo kutoka kwa wananchi waliochukua jukumu la
kuwabeba watoto na kuwapeleka katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata
“Leo majira ya saa nne asubuhi niliwapokea wananchi
kutoka mtaa wa Bugwandege walifika wakiwa wameongozana na mama mmoja pamoja na
watoto wake wawili wakaeleza kuwa baada ya watoto hao kuwaona wanaendelea
kuishi bila msaada”.
Diwani
wa kata ya Ibinzamata Mheshimiwa Ezekiel Sabo amekemea kutokea kwa tukio hilo
huku akiwaomba wananchi wa kata hiyo kuacha tabia ya kutoa adhabu kali kwa
watoto wao,kwani kwa kufanya hivyo ni ukatili.
“Taarifa hii ya watoto kuchomwa moto nimeipokea kwa
masikitiko makubwa sana lakini nakemea swala hili lisijitokeze tena katika kata
ya Ibinzamata kwa sababu jamii ikifikia hapo basi tutakuwa tumefika pabaya sana
na niviombe vyombo vya serikali vifuatilie ili ukatili huu usijirudie tena”.amesema diwani Sabo
Msaidizi
wa kisheria kutoka Community Edification Organization kata ya Ibinzamata Robert
Said amesema kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.
Post a Comment