Wananchi wa Vijiji
vitano vya Ikinabushu, Isuyu, Nyawa, Mwauchumu na Gilya Kata ya Gilya Wilaya ya
Bariadi Mkoani Simiyu wanatarajia kunufaika na mradi wa Umeme unatekelezwa na
Serikali kupitia mkandarasi Sengerema Engeniering Group.
Meneja wa TANESCO Mkoa
wa Simiyu Alistedia Clemence amesema mkandarasi huyo anatekeleza mradi huo
katika vijiji 52 vya wilaya ya Bariadi na kwamba tayari ameshawasha umeme
katika vijiji 27 na bado vijiji 25.
Amesema kuwa mkandarasi
huyo anatekeleza miradi ya umeme katika Wilaya za Bariadi, Itilima na Busega kwa
gharama ya shilingi bil. 30.
Ameongeza kuwa ujenzi
huo unatarajia kukamilika mwezi Juni
mwaka huu, huku akiwataka wananchi kuunganisha umeme majumbani kwa gharama ya
shilingi 27,000/- pia kutunza miundombinu ya umeme.
Mkuu wa wilaya ya
Bariadi Lupakisyo Kapange amewataka wananchi kutochoma moto nguzo za Umeme na
kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Amesema miradi ya
Maendeleo ikiwemo umeme inaletwa na Serikali Kwa ajili ya kuharakisha maendeleo
ya wananchi kiuchumi na kijamii ambapo kupitia umeme wanaweza kuanzisha
Biashara.
Post a Comment