Hali ya Mtoto akiwa Hospitalini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda. |
Na Derick Milton Simiyu.
Siku moja baada ya blog ya Simiyupressblog kutoa taarifa za mtoto (7) kufanyiwa vitendo vya ukatili na Baba yake anayedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi Bariadi Mkoani Simiyu.
Hatimaye Jeshi la Polisi Mkoani hapa, limejitokeza mbele ya waandishi wa Habari na kuzungumza tukio la mtoto huyo (jina linahifadhiwa) ambaye alipigwa hadi kujeruhiwa na Baba yake anayediwa kuwa Askari Polisi kituo cha Polisi Bariadi.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Blasius Chatanda amesema kuwa ni
kweli Baba wa mtoto aliyefanya ukatili huo ni Askari wa jeshi hilo, katika
kituo cha Polisi Bariadi na anashikiliwa jeshi hilo.
Kamanda Chatanda amesema kuwa wanamshikilia Askari huyo mwenye namba PC H.4178, Abati Benedicto
Nkalango (27) kwa kosa la kumpiga mtoto wake na kumsababishia vidonda sehemu
mbalimbali za mwili.
Chatanda amesema kuwa askari huyo alimpiga mtoto wake wakati
akikagia madaftari ya Shule.
"Mnamo tarehe 15/1/2023,.Majira ya saa 11:00 huko katika
kambi ya Kituo Cha Polisi Wilaya ya Bariadi, Askari wa Jeshi la Polisi namba PC
H.4178 Abati Benedicto Nkalango (27), msukuma, alimshambulia mtoto wake aitwaye
Benedicto Abati (7) mwanafunzi wa Shule ya msingi Gappa Kwa kumpiga na fimbo
sehemu mbalimbali za mwili wake na kimsababishia majeraha makubwa" amesema
Chatanda.
Soma zaidi.......https://simiyupresstz.blogspot.com/2023/01/askari-polisi-adaiwa-kumfanyia-vitendo.html
Post a Comment