Askari Polisi adaiwa kumfanyia vitendo vya ukatili Mtoto wake (7)

 

Mtoto aliyefanyiwa ukatili na Baba yake anayedaiwa kuwa ni Askari Polisi.




Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Somanda Dr. Emmanuel Costantine.


Na Derick Milton Bariadi.

 

Mtoto mmoja (Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 7 anayesoma katika Shule moja ya shule binafsi ya mjini Bariadi Mkoani Simiyu amefanyiwa kitendo Cha ukatili wa kipigo na baba yake kwa madai kuwa hajui kusoma na kuandika.


Taarifa ambazo hajidhibitsihwa ni kuwa Baba wa mtoto huyo ni Askari Polisi kituo cha Polisi Bariadi.


Baada ya uwepo wa taarifa za mtoto huyo, Mwandishi wa Habari hii alifika Hospitali ya Mji wa Bariadi (Somanda) na kukuta mtoto huyo akipatiwa matibabu.


Mtoto huyo alikutwa na majeraha sehemu za mgongo, kichwa na masikioni ambapo imeonekana pia kuwa alikuwa na majeraha makubwa ambayo ni mapya na mengine ya muda mrefu.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi (Somanda), Dr. Emmanuel Costantine aliwaambia waandishi wa habari kuwa January 19, Majira ya saa 4:00 asubuhi walimpokea mtoto huyo kwa ajili ya matibabu.


" Tulimpokea mtoto huyu akiwa na majeraha mapya na ya zamani (anataja jina lake), ni wa kiume miaka 7 na mkazi wa malambo anasoma darasa la 1 shule ya msingi (anaitaja) amelazwa wodi ya watoto na anaendelea na matibabu" anasema Dr. Costantine.

 

Mama mlezi wa mtoto huyo, (jina limahifadhiwa) mkazi wa malambo amesema mtoto huyo alipigwa na baba yake ambaye alimtaja kuwa ni askari Polisi kwa kosa la kutokuandika shuleni.

 

Anasema  mtoto huyo alipigwa na baba yake siku ya jumapili (January 15, 2023), na kwamba walimpeleka shuleni siku ya Alhamisi ambapo baada ya walimu kumdadisi ilibidi aeleze ukweli.

 

"Naishi pamoja na mwanaume huyo ambaye alimpiga, mimi ni mke wake na huyo mtoto siyo wa kwangu bali ni mtoto wa mke mwenzagu …. Nami sikufurahishwa na kitendo hicho" anasema ….

 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ambako mtoto huyo anasoma (jina linahifadhiwa) alisema mtoto huyo alikuwa amesajiliwa kusoma darasa la kwanza katika Shule hiyo.

 

Anasema  Mahudhurio ya kijana huyo yalikuwa hafifu, Kwani siku ya jumatatu, jumanne na jumatano hakuhudhuria masomo.

 

"aliletwa na mama yake wa kambo, akiwa amechelewa saa za masomo, Mwalimu alimwona haandiki, hana raha, alipomuuliza, akasema..." Anaeleza Mwalimu Mkuu

 

"Mwalimu  wa darasala alichukua uhamuzi wa kumuita mwalimu mlezi (patron), Wakamwingiza chumba maalum kumkagua, wakakuta mtoto huyo ana majeraha yasiyokuwa ya kawaida"

 

Anasema, baada ya walimu kuona Hali hiyo, walimwita Mwalimu Mkuu na bahati nzuri mama mlezi alikuwa Bado yuko shuleni ambapo walimbana na kuwaeleza ukweli kuwa kapigwa na baba yake mzazi kwa kutumia waya.

 

"Niliitwa, tukambana yule mama wa kambo, akakiri kuwa alipigwa na baba yake kwa waya, akasema anampiga sababu anamfundisha,.."

 

Mwalimu Mkuu huyo amesema kuwa walimchukua mtoto huyo, mama mlezi pamoja na mwalimu mlezi kuelekea Kituo Cha polisi mjini Bariadi, lakini wakiwa njiani alipigwa simu na baba yake na mtoto juu ya hali ya mtoto, ambapo Baba mzazi limtaka Mwalimu Mkuu huyo wayamalize na asimpeleke mtoto kituo cha Polisi.

 

" Wakati tunaelekea Kituoni, Baba wa mtoto aliniomba msamaha kwa njia ya simu akinitaka tuyamalize, nami nilikataa kutokana na hali ya mtoto alivyokuwa ameumia”

 

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Janeth Jackson amekiri kupata tukio hilo huku akieleza kuwa kesi imesharipotiwa jeshi la Polisi.

 

"Sisi kama Ustawi wa jamii tunahusika zaidi na mtoto Kwa sababu ni kosa ambalo kalifanya baba na kesi yake iko Polisi na sisi tunahakikisha mtoto anapata matibabu hospitalini" amesema na kuongeza.


 "Kuhakikisha anapona majeraha yake na pia kumtafuta mtu stahiki ambaye atamlea na kuhakikisha Ulinzi na Usalama wake"


Hata hivyo taarifa zilieleza kuwa Baba mzazi wa mtoto huyo alikamatwa na kuwekwa rokapu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakusema chochote.


MWISHO.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post