Msako wa nyumba kwa nyumba uliofanywa na Viongozi wa Kata ya Izumacheli umezaa matunda baada ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 40 wa shule ya Sekondari Izumacheli kuripoti shuleni.
Hatua hii imekuja baada ya siku chache Katibu Tawala Wilaya ya Geita Thomas Dime kufanya ziara katika shule ya Sekondari Izumacheli na kukuta mwitikio usioridhisha wa wanafunzi ambapo wa kidato cha kwanza walikuwa wanne tu kati ya Wanafunzi 88 waliopaswa kuripoti shuleni hapo kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza.
Chanzo Star tv. https://www.instagram.com/p/CneebyvqLRm/
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق