Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo Cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 akitoka mahakani baada ya kukosa dhamana. |
Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo Cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 akitoka mahakani baada ya kukosa dhamana. |
Na Derick Milton, Bariadi.
Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo Cha
Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi
kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 jana amefikishwa katika mahakama
ya Wilaya ya Bariadi kujibu mashtaka yanayomkabili.
Ikumbukwe taarifa za Askari huyo kumfanyia vitendo
vya kikatili mtoto wake, zilianza kuripotiwa katika vyombo vya habari baada ya tukio la Januri 15, 2023 la kumpiga
mtoto wake maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumjeruhi vibaya.
Januari 23, 2023 Jeshi la Polisi kupitia taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Blasius Chatanda kwa waandishi wa
Habari walikiri askari huyo kutenda tukio hilo na kueleza kuwa wanamshikilia
kwa uchunguzi zaidi.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mariam
Nyangusi askari huyo alisomewa mashataka yanayomkabili na mwendesha mashtaka wa
serikali Daniel Masambu ambayo ni kufanya ukatili dhidi ya mtoto.
Kesi hiyo namba 8/2023 ikisomwa kwa mara ya kwanza
mwendesha mashtaka alieleza Mahakama kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa Hilo January 15, 2023 katika
eneo la line polisi lililopo mtaa wa malambo mjini Bariadi.
Masambu alieleza kuwa mtuhumiwa alimchapa mtoto
wake kwa fimbo na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili wake kinyume na kifungu
Cha 169 A kifungu kidogo Cha 1 na Cha 2 Cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2022.
Hata hivyo mtuhumiwa alikana kosa hilo na kuelezwa
na Hakimu kuwa dhamana yake iko wazi kwa
masharti ya kuwa na fungu la dhamana ya sh. Mil 3 na wadhamini wawili wenye
vitambulisho.
Mwendesha mashtaka alieleza mahakama kua tayari upelelezi umekamilika na kesi hiyo kupangwa
kuanza kusikilizwa hoja za awali March 2 mwaka huu 2023.
Hata hivyo Mtuhumiwa hakutimiza vigezo vya kupata
dhamana na amerudishwa rumande.
Mwisho.
Post a Comment