Mkandarasi SGR alivyoibiwa Lori, lakamatwa Tabora likitafutiwa mteja.

Gari (Lori) lenye namba za usajili T.344 DXM aina ya HOWO tani 12 lenye thamani ya Sh. Milioni 180 mali ya Kampuni ya  ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), likiwa kituo cha Polisi Maswa baada ya kukamatwa likiwa Mkoani Tabora kwenye harakati za kuuzwa mara baada ya kuibiwa kwa mkandarasi wa SGR.
 



Na Derick Milton, Bariadi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Jeshi la Polisi mkoani Simyu limefanikiwa kulikamata gari (Lori) lenye namba za usajili T.344 DXM aina ya HOWO tani 12 lenye thamani ya Sh. Milioni 180 mali ya Kampuni ya  ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).


Gari hilo inadaiwa liliibiwa katika kambi ya ujenzi wa Kampuni hiyo iliyopo Kijiji cha Malampaka Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, ambapo lilikamatwa likiwa Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wahusika wakiwa katika haraka za kutafuta wateja kwa ajili ya kuliuza.


Hata hivyo jeshi hilo halikufanikiwa kuwakamata watu waliohusika kuiba Roli hiyo, ambapo uchunguzi unaendelea kwa ajili ya kubaini wahusika.


Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Blasius Chatanda amesema kuwa mabaini matukio ya wizi katika mradi huo yanaanzia ndani ya kampuni hiyo.


wakati huo huo Watu 17 wamekamatwa na Jeshi la hilo kwa kuhusika katika vitu mbalimbali katika mradi huo wa SGR Kambi ya Malampaka iliyoko Wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani humo Blasius Chatanda amesema kuwa baadhi ya vitu vilivyoibiwa katika mafuta Lita 560 Dizeli.


Vitu vingine mifuko ya saruji 79, mirija ya kunyonyea mafuta mafuta 21, Baiskeli 8, Mabomba ya chuma 19, madumu tupu 20, wavu 10 za aina mbalimbali Mapipa tupu 02, Nondo vipande 04, vipande 05 vya red Copper.


Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa ukamataji wa watu hao pamoja na mali hizo, umefanyika katika opereisheni kubwa ambayo inaendelea kwenye mradi huo, ikihusisha mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post