Na Derick Milton, Bariadi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Jeshi la Polisi mkoani
Simyu limefanikiwa kulikamata gari (Lori) lenye namba za usajili T.344 DXM aina
ya HOWO tani 12 lenye thamani ya Sh. Milioni 180 mali ya Kampuni ya ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).
Gari hilo inadaiwa liliibiwa katika kambi ya
ujenzi wa Kampuni hiyo iliyopo Kijiji cha Malampaka Wilayani Maswa Mkoani
Simiyu, ambapo lilikamatwa likiwa Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wahusika
wakiwa katika haraka za kutafuta wateja kwa ajili ya kuliuza.
Hata hivyo jeshi hilo halikufanikiwa kuwakamata watu waliohusika kuiba Roli hiyo, ambapo uchunguzi unaendelea kwa ajili ya kubaini wahusika.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Blasius Chatanda amesema
kuwa mabaini matukio ya wizi katika mradi huo yanaanzia ndani ya kampuni hiyo.
wakati huo huo Watu 17 wamekamatwa na Jeshi la hilo kwa kuhusika katika vitu mbalimbali katika mradi huo wa SGR Kambi ya Malampaka iliyoko Wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa
Polisi Mkoani humo Blasius Chatanda amesema kuwa baadhi ya vitu vilivyoibiwa
katika mafuta Lita 560 Dizeli.
Vitu vingine mifuko ya saruji 79, mirija ya kunyonyea mafuta mafuta 21, Baiskeli 8, Mabomba ya chuma 19, madumu tupu 20, wavu 10 za aina mbalimbali Mapipa tupu 02, Nondo vipande 04, vipande 05 vya red Copper.
Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa ukamataji wa watu hao pamoja na mali hizo, umefanyika katika opereisheni kubwa ambayo inaendelea kwenye mradi huo, ikihusisha mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga.
إرسال تعليق