Maadhimisho Siku ya kifua kikuu Simiyu, Kila mwanachi kupata Chakula bure.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) ofisni kwake leo

 

Na Derick Milton, Simiyu.


Uongozi wa Mkoa wa Simiyu, umewataka wananchi wake kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, ambayo kitaifa yatafanyika mkoani humo katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.


Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda amesema kuwa siku hiyo, kutatolewa Chakula na kila mwananchi atakula na kushiba na kwamba wamejiandaa kuhakikisha kila atakayehudhuria anapata huduma hiyo bure.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo juu ya maadhimisho hayo, Dkt. Nawanda amesema kuwa mbali na huduma ya Chakula kutakuwepo na huduma nyingine ikiwemo upimaji wa ugonjwa huo.


“ Serikali ya Mkoa imeandaa Chakula kwa kila mwananchi ambaye atahudhuria maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Halmashauri ya Mji, kila mtu atakula na kusaza, tumeandaa chakula cha kutosha wananchi waje, itakuwa siku ya maadhimisho na kula” amesema Dkt. Nawanda.


Amesema kuwa mgeni rasmi takuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo maelezea maandalizi kuwa yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza wingi kuweza kushiriki maadhimisho hayo.


Amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “ kwa pamoja tunaweza kutomeza kifua kikuu nchini Tanzania” ambapo amewataka wadau wote kwa pamoja kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.


MWISHO.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post