Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) ofisni kwake leo |
Na Derick Milton, Simiyu.
Uongozi wa Mkoa wa Simiyu, umewataka wananchi wake
kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, ambayo
kitaifa yatafanyika mkoani humo katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda amesema kuwa
siku hiyo, kutatolewa Chakula na kila mwananchi atakula na kushiba na kwamba
wamejiandaa kuhakikisha kila atakayehudhuria anapata huduma hiyo bure.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake
leo juu ya maadhimisho hayo, Dkt. Nawanda amesema kuwa mbali na huduma ya
Chakula kutakuwepo na huduma nyingine ikiwemo upimaji wa ugonjwa huo.
“ Serikali ya Mkoa imeandaa Chakula kwa kila
mwananchi ambaye atahudhuria maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Halmashauri ya
Mji, kila mtu atakula na kusaza, tumeandaa chakula cha kutosha wananchi waje,
itakuwa siku ya maadhimisho na kula” amesema Dkt. Nawanda.
Amesema kuwa mgeni rasmi takuwa Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, ambapo maelezea maandalizi kuwa yamekamilika na kuwataka wananchi
kujitokeza wingi kuweza kushiriki maadhimisho hayo.
Amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “ kwa
pamoja tunaweza kutomeza kifua kikuu nchini Tanzania” ambapo amewataka wadau
wote kwa pamoja kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
MWISHO.
إرسال تعليق