Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam. Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Mwenyekiti wa Bodi TGNP, Gemma Akilimali akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada Bi.Helen Fytche akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden Bi.Nasieku Kisambu akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam. Mwakilishi Mkazi UN Women Bi.Hodan Addou akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI katika kuzindua taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya ukatili wa watoto mtandaoni nchini, matokeo yanaonesha kuwa asilimia 4% ya watumiaji wa mtandao wenye umri wa miaka 12-17 nchini Tanzania ni manusura wa ukatili wa mitandaoni.
Hayo yamesemwa leo Machi 9,2023 na Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
Amesema katika matokeo ya utafiti huo inaonesha wengi hufanyiwa ukatili kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram, Facebook na TikTok.
"Tunatambua pia kuwa Serikali yetu imetunga sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa lengo la kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mitandao na vifaa vya kiteknolojia",amesema.
Aidha wameiomba Serikali iimarishe utekelezaji wa sheria zilizopo na itunge kanuni ambazo zitakuwa na mrengo wa kijinsia kwa ajili kutoa ulinzi maalumu kwa watoto wa kike dhidi ya unyanyasaji wa kimtandao.
"Kipekee, tunaomba Wizara husika pamoja na mamlaka kuendelea kusimamia usalama wa watumiaji wa mitandao na kuchukua hatua pale ambapo udhalilishaji unajitokeza ili kusaidia kujenga jamii inayoheshimu utu wa mtoto wa kike na mwanamke", amesema.
Pamoja na hayo amesema ushiriki wa wanawake katika tasnia ya sayansi na teknolojia bado ni mdogo hivyo hamasa zaidi inapaswa kuendelea kutolewa ili kuongeza idadi hiyo.
Amesema miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kushiriki katika kampeni mbalimbali za kuleta hamasa ikiwemo Siku ya wanawake na watoto wa kike katika tasnia ya sayansi na teknolojia, inayoadhimishwa kila mwaka Februari 11.
"Ninatambua juhudi zinazofanywa na vyuo vikuu na vyuo vya kati vya humu nchini pamoja na makundi mbalimbali amabo wamekuwa wakihamasisha wanafunzi wa kike kwenye masomo ya sayansi teknolojia uhandisi na hisabaai na kushiriki kwenye bunifu mbalimbali ikiwemo na mashindano yanayo andaliwa na wizara ya Elimu sayansi na teknolojia, na Tume ya sayansi na Teknolojia COSTECH",ameeleza.
Hata hivyo amewapongeza TGNP kwa kuwa kinara katika kutumia teknolojia katika kuimarisha usawa wa kijinsia kwa kutengeneza mifumo mbalimbali, kuwaandaa na kuwahamasisha watoto wa kike kuingia kwenye tasnia ya Sayansi na teknolojia kupitia majukwaa huru na salama ya wanawake na vilinge vya simulizi, pamoja na majukwaa mbalimbali ambayo pia yamekuwa yakijadili changamoto zitokanazo na maendeleo ya teknolojia hususani ukatili wa kijinsia.
Vilevile ametoa wito kwa wanawake viongozi na wenye fani mbalimbali kuweza kuajiandikisha katika kanzidata ya taifa ya wanawake ijulikanayo kama Women Connect Portal ambayo itasaidia wanawake husika kujulikana na pia wasichana wanaochipukia na vizazi vijavyo, kuweza kujifunza na kupata hamasa kutoka kwa wanawake hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi TGNP, Dada Gemma Akilimali amesema kuwa taarifa ya UN Women Gender Snapshots (2022) inaonesha kuwa kutokuwepo kwa wanawake katika ulimwengu wa kidijitali kumepoteza dola za Kimarekani Trilioni moja katika pato la taifa kwa nchi zenye uchumi wa chini na wa kati kwa muongo uliopita, hasara ambayo inatarajiwa kukuwa hadi kufikia Dola za Kimarekani Trilioni 1.5 ifikapo 2025,
Amesema taarifa hiyo imesisitiza kuwa kutokomeza hasara hiyo, nchi hazina budi kuweka nguvu katika kutokomeza ukatili wa kimtandao, ambao utafiti uliofanywa kwa nchi 51, ulionesha kuwa asilimia 38 ya wanawake wamekutana na ukatili huo wao kama wao.
"Imedhihirika kuwa kuwawezesha wanawake na makundi mengine kushiriki katika eneo la teknolojia ina matokeo chanya hasa katika ubnifu wa suluhisho za changamoto mbalimbali za kijamii na uvumbuzi mwingine unaowasaidia wanawake na watoto wa kike kupata mahitaji yao na hivyo, kuchochea ufikiwaji wa usawa wa kijinsia",amesema
Naye Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi amewaasa mabinti wa kike na wanawake kwa ujumla kuacha kuweka mitandaoni picha za utupu kwani kwa kufanya hivyo pia ni kuchochea ukatili kwa watoto wa kiume na wanaume na kuwapa matamanio yasiyo na ulazima.
"Unapoweka picha za utupu leo ukumbuke kuwa zitaendelea kukaa huko na ipo siku zitatumika kukuangusha pale unapotafuta fursa au kazi au kujaribu kugombea nafasi ya uongozi". Amesema Bi.Liundi.
Bi. Liundi amesema kuwa TGNP kwa kushirikiana na wadau wake, wanaratibu shughuli mbalimbali katika kipindi chote cha mwezi huu wa tatu ambapo Vituo vya Taarifa na Maarifa 35 kutoka mikoa 10 Tanzania inafanya maadhimisho kati ya tarehe 1 hadi 31 Machi.
Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akiwa pamoja na Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi na wadau wengine wakimsikiliza mmoja wa wabunifu wanawake wakionesha ubunifu wao katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Mgeni Rasmi Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja (katika) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi TGNP, Dada Gemma Akilimali na Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi wakiburudika kucheza muziki pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi (wa kwanza mwenye miwani) akiburudika kucheza muziki pamoja na mabinti wa kike katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.Baadhi ya mabinti wakiburudika kucheza muziki pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya mabinti wakicheza muziki pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam. Baadhi ya mabinti wakiburudika kucheza muziki pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akiwa na Mwenyekiti wa Bodi TGNP, Dada Gemma Akilimali (kulia kwake) na Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kushoto kwake) wakipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam. Mgeni Rasmi Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akiwa na Mwenyekiti wa Bodi TGNP, Dada Gemma Akilimali (kulia kwake) na Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi (kushoto kwake) wakipata picha ya pamoja na wadau wa TGNP katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 9,2023 yanayoendelea kwa siku mbili katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق