Na Mwandishi wetu, Simiyu.
Kampuni ya mabasi
ya Ally’s Star ya Mkoani Shinyanga imepewa onyo la mwisho na uongozi wa Mkoa wa
Simiyu, kwa kile kilichodaiwa kutoa huduma mbaya kwa wateja wake ikiwemo lugha
zisizokuwa na staha kwa abiria.
Kampuni hiyo
ambayo baadhi ya magari yake ya kubeba abiria (basi) ufanya safari zake kutoka
Mkoani Simiyu (Bariadi) hadi Dar es Salaam, ambapo abiria kutoka mkoani Simiyu
wamekuwa wakilalamikia juu ya huduma mbovu za magari hayo.
Moja ya kero
kubwa inayodaiwa kulalamikiwa abiria wengi ni suala la kufaulishwa bila ya utaratibu,
huku ikiambatana na lugha mbaya endapo abiria wanapoonza kulalamikia utaratibu
huo.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Dkt. Yahya Nawanda jana kwenye maazimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
Barabarani yaliyofanyika mjini Bariadi, alitoa onyo la mwisho kwa kampuni.
Dkt. Nawanda
alisema kuwa ikiwa Kampuni hiyo wataendeleza utaratibu huo watapigwa marufuku
kufanya kazi mkoani humo, kwa kile alichoeleza kuwa malalamiko kwake yamekuwa
mengi.
Alisema kuwa baadhi
ya magari ya kampuni hiyo ufanya safari zake kutoka Bariadi kwenda Dodoma na
Morogoro, ambapo wakati wa kutoka kwenye mikoa hiyo kuja Bariadi abiria hao
ukalishwa Mkoani Shinyanga wakisubilia basi la kampuni hiyo kutoka Dar es
Salaam.
“ Watu wanatoka
Morogoro na Dodoma kuja Bariadi, wakifika Shinyanga saa 10:00 jioni,
wanakalishwa Shinyanga mpaka saa nne usiku wakisubilia basi la kampuni hiyo
kutoka Dar es salaam” alisema Dkt. Nawanda….
“ Wanawakalisha
Shinyanga muda mrefu…kwanza wanawapotezea muda, lakini abiria hawapewi chakula
wala chai kama ilivyosheria, abiria wakianza kulalamika wanatolewa lugha mbaya”
aliongeza Dkt. Nawanda.
Mkuu huyo wa Mkoa
aliagiza Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Mkoani humo kufanya
uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na kumchukulia hatua kali mmiliki wa magari hayo.
“ Waambieni
wahusika, waache mara moja hii tabia, malalamiko sasa yamekuwa mengi, ikiwa
wataendelea nitachukua hatua kali ya kuwazuia kufanya biashara kwenye mkoa huu,
hatuwezi kuwa na watu wanaonyanyasa wananchi,” alisema Dkt. Nawanda.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga naye alisema kuwa amepata malalamiko ya magari ya kampuni hiyo ambapo alimtaka mmilikiwa wa magari hayo kujirekebisha mara moja.
“ Kila mmoja
amemsikia mkuu wa Mkoa akisema atawazuia kufanya kazi ndani ya mkoa ikiwa
wataendelea, sasa mimi nasema kabla ya Mkuu wa Mkoa kufanya hivyo, mimi
nitawapiga marufuku kufanya kazi ndani ya Wilaya ya Bariadi”
“ Nimsihi mmiliki
wa haya magari, kama anaipenda kazi yake basi aache mara moja huu utaratibu,
mimi huwa sishindwi jambo, nikiamua nafanya kweli, narudia tena waache mara
moja” aliongeza Simalenga.
Ofisa mfawidhi
kutoka LATRA Mkoani humo Niclous Kamzora alikiri ofisi yake kupata malalamiko
kutoka kwa abiria dhidi ya magari ya magari ya kampuni hiyo na walianza
kuyafanyia kazi.
“ Tulipata hayo
malalamiko, tukamwandikia barua ya onyo na tukimtaka atoe maelezo, sasa leo
Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwetu, na inavyoonekana kampuni hii imerudia
makosa, tunakwenda kufuatilia na ikibainika tutachukua hatua kali,” alisema
Kamzora.
Hata hivyo
tulimtafuta msimamizi wa Magari hayo Abdallah Abdallah ambaye alisema kuwa tuhuma
hizo dhidi ya kampuni yao hazina ukweli, bali ni vita ya kibiashara kutokana na
ukubwa wa kampuni yao.
Abdallah alisema
kuwa siyo kweli kuwa abiria ufaulishwa kila mara, bali utokea mara moja ikiwa
gari moja likipata itirafu ya kiufundi, basi abiria utakiwa kusubilia gari
nyingine ili waweze kufikishwa salama.
“ Hili jambo ni
mara moja tu, hatuwezi kusafirisha abiria na gari mbovu, tukiona hili gari
limekuwa na itilafu, basi tunawaomba abiria kusubilia gari lililoko nyuma ili
kuwafikisha salama” alisema Abdallah…
“ Suala la lugha
mbaya nalo siyo kweli, ndiyo maana magari yetu mpaka sasa yanapata abiria wengi
kutoka Bariadi, waswahili walitufundisha wakasema hivi…ukoo mkubwa na misiba
mingi…Asante” alisema Abdallah.
MWISHO.
إرسال تعليق