
Na Bahati Sonda, Simiyu.
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu
wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria
unaotekelezwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 440 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
iliyotolewa na aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Dkt John Joseph Magufuli.
Ikumbukwe kuwa mradi huo umesubiriwa
kwa muda mrefu na wananchi wa Mkoa wa Simiyu hatimaye leo wameweza kushuhudia
utiaji saini mradi huo ambao unatekelezwa na Serikali awamu ya sita chini
ya Uongozi wa rais Samia Suluhu ambao utakwenda kuzinufaisha Wilaya zote 5 za
Mkoa wa Simiyu hivyo kuwawezesha wananchi kuepukana na adha ya upatikanaji wa
maji safi na salama.
Hayo yamebainishwa mapema leo na Waziri
wa Wizara Maji Jumaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu
mara baada ya utiaji saini mkataba wa mradi huo ili kazi iweze kuanza na
kuwahakikishia wanasimiyu kuwa hakuna mtu yeyote atakayekwamisha mradi huo na
kwamba kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa watahakikisha unakamilika kwa wakati
hivyo kupata huduma hiyo muhimu.
Awesso ameongeza kuwa wakati rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia bunge alitoa maelekezo mahususi kwa
Wizara ya maji kuwa wanaokumbana na adha ya maji ni kinamama hivyo hataki kuona
wakikumbana na changamoto hiyo na kuongeza kuwa mradi huo utawanufaisha
Wanasimiyu kwenye masuala ya kilimo pamoja na ufugaji.
Aidha Waziri huyo ametoa rai
kuwa mradi huo utekelezwe kwa pamoja badala ya kutekelezaa kwa awamu kwani
suala la maji halina mbadala huku akiwahakikishia vijana wa Mkoa huo kunufaika
na ajira pindi mradi utakapokuwa unatekelezwa.
"Tunakwenda kutekeleza mradi
huu kwa pamoja sitaki kusikia unatekelezwa kwa awamu ili kuhakikisha wananchi
wanapata maji safi na salama na yenye kuwatosheleza hivyo kazi yetu sisi
viongozi wa Wizara jukumu letu ni kutafuta fedha kushirikiana na wadau wetu na
tutafanya kila linalowezekana ili tufikie adhma ya kumtua mama ndoo kichwani na
kwamba lengo letu kufikia 2025 upatikanaji wa maji vijijini uwe umefikia 85% na
mjini 95%"Amesisitiza Awesso
Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt
Yahaya Nawanda amesema kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa
inayotekelezwa na awamu ya sita na kwamba kwa awamu ya kwanza unatarajiwa
kuwanufaisha takriban wananchi 400,000 na kumhakikishia Waziri wa maji kuulinda
kwa nguvu zote sambamba kuwahakikishia ushirikiano wakandarasi watakaokuwa
wanatekeleza mradi huo.
Sambamba na hayo Dkt Nawanda
ameeleza kuwa katika bajeti ya mwaka 2023/2024 jumla ya miradi 29 inaenda
kutekelezwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 kwa hivyo kuongeza hali
ya upatikanaji wa maji katika Mkoa kutoka 72% hadi kufikia 79% na kwamba kwa
kipindi cha mwaka 1 umefanikiwa kuongeza upatikanaji wa maji 3.78.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji
Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha
wakazi wa Simiyu wanapata maji kwa 100% serikali hapa nchini kupitia
Wizara ya Maji inatekeleza mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia .
Aisha ameongeza utapeleka huduma ya
maji ya uhakika kwa kuboresha na kupanua mfumo wa usambazaji maji kwenye Wilaya
zote na kwamba utahusisha ukarabti na ujenzi wa mabwawa ya kilimo endelevu cha
umwagiliaji utakaotumika kupunguza adha ya maji kwa ajili ya kilimo na mifugo
na ununuzi wa mbegu bora na uanzishwaji wa mashamba darasa.


Post a Comment