TCA yawapatia Wakulima wa Pamba Matrekta 200.

MATREKTA kwa ajili ya shughuli za Kilimo.

 

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

CHAMA Cha Wanunuzi wa Pamba nchini (TCA) kimetoa Matrekta 200 kwa wakulima wa Pamba na mazao mengine ili waweze kulima kwa wakati, waongeze tija na pia waachane na jembe la mkono.

 

Matrekta hayo ambayo yatagawiwa kwa wakulima nchini, kutoka kampuni ya Agricom, yatalenga kuwanufaisha wakulima, ili waweze kulima kwa wakati na kufikia lengo la serikali la kuwakwamua kiuchumi.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa TCA nchini, Boaz Ogolla amesema wanunuzi hao wamejiandaa kuwahudumia wakulima ili kuongeza tija baada ya kuhamasishwa na Waziri wa Kilimo (Hussein Bashe).

 

‘’Wanunuzi wa Pamba, Tulichanga fedha kwa ajili ya kuwa hudumia wakulima, tumenunua Matrekta 200 kupitia Mfuko wa kuendeleza zao la Pamba…wiki hii tutasambaza Trekta 100 na wiki ijayo tutasambaza pia Trekta 100, lengo ni kuwalimia wakulima kwani wakati wa kilimo hawana zana za kisasa’’ amesema Ogolla.

 

Ameeleza kuwa wakulima wengi wanategemea jembe la mkono na jembe la kukokotwa na wanyamakazi (plau) ambao wakati wa kilimo hukosa malisho na kusababisha kuchelewa kulima na pia kulima kwa mkono hutumia muda mrefu.

 

Amesema Trekta hizo zitawasaidia wakulima kwa wakati, kwa bei nafuu na pia zitawafikia vijijini kwa wakati na wakulima ambao hanawa fedha watakopesha kupitia utaratibu wa kilimo mkataba ili waweze kurejesha na endapo wakifanikiwa wataongeza Matrekta mengi mwaka ujao.

 

Katika hatua nyingine Ogolla ameipongeza serikali kupitia Boadi ya Pamba (TCB) kwa kutoa ndege zisizokuwa na rubani (drone) kwa ajili ya kupuliza mashamba makubwa ya wakulima ili kudhibiti wadudu waharibifu wa zao la pamba.

 

‘’Mkulima anachoka akitumia pampu ya mgongoni, Bodi ya Pamba imerahishisha upuliziaji ili kukabiliana na wadudu wanaotuharibia pamba…mkulima mwenye ekari 100 hawezi kudhibiti wadudu kwa wakati mmoja’’ amesema Ogolla.

 

Amesema, mbali na kununua Trekta pia watanunua mashine kubwa ya kupulizia wadudu shambani (Pressure pump) ili kurahisisha upuliziaji na kudhibiti wadudu wasiweze kuharibu zao la pamba.

 

Kwa upande wake Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Pamba, Renatus Luneja amesema baada ya serikali kugawa pikipiki kwa maafisa ugani, zimechangia kuimarisha huduma za ugani.

 

‘’Sisi tunaona pikipiki zimesaidia kuimarika kwa huduma za ugani, kilichobaki ni kuimarisha usimamizi wa watoa huduma za ugani…mfano elimu ya upandaji wa sentimita 60 x setimita 30 imeenea walau kufikia asilima 70 kwa mkoa wa Simiyu’’ amesema.

 

Ameongeza kuwa kutokana na serikali pamoja na wadau wa kilimo kuboresha kwa huduma za ugani, upandaji wa kuzingatia vipimo hivi utaongeza tija katika uzalishaji wa pamba.

 

MWISHO.


 


Katibu wa Chama Cha Wanunuzi wa Pamba nchini (TCA), Boaz Ogolla akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ununuzi wa Matrekta 200 kwa ajili ya kuhudumia wakulima.

 

Matrekta kwa ajili ya shughuli za Kilimo.


Trekta yenye mtambo maalumu kwa ajili ya kupakia Pamba kwenye tela.


Zao la Pamba.


Ndege isiyokuwa na Rubani (drone) iliyotolewa na Bodi ya Pamba (TCB) kwa ajili ya kupulizia wadudu amshamba ya wakulima wa Pamba.


Ndege isiyokuwa na Rubani (drone) iliyotolewa na Bodi ya Pamba (TCB) kwa ajili ya kupulizia wadudu amshamba ya wakulima wa Pamba.

 

Mkulima wa Pamba, mkazi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima akipulizia dawa shambani.


Mkulima wa Pamba, mkazi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima akipulizia dawa shambani.

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post