Majambazi yavamia maduka ya fedha Bariadi, walifunga Barabara zote.

Maduka katika mtaa wa Sokoni, halmashuari ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambayo yalivamiwa na Majambazi jana usiku.


Na Mwandishi wetu, Bariadi.


Watu kadhaa wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na siraha mbalimbali wamevamia maduka yanayofanya Biashara za miamala ya kifedha ambalo limetokea majira ya saa Saba usiku wa kuamkia Leo.


Maduka yaliyovamiwa ni katika mtaa wa sokoni katikati ya Mji wa Bariadi, ambapo wavamizi walivunja milango na kufanikiwa kuingia ndani lakini walishindwa kuvunja boski za kuhifadhia fedha (Seif) ambazo ndizo walikuwa wamezilenga.

Inadaiwa waarifu hao, walifunga Barabara zote zinazoingia eneo ambako maduka yalipo, huku walinzi wakikimbia baada ya kutishiwa kuuawa.

Baadhi ya wananchi ambao ni majirani kwenye maduka hayo, wamesema kuwa usiku majira ya saa Saba walisikia milio ya risasi kati ya askari pamoja na watu hao waliosadikika kuwa majambazi.

Mmoja wa walinzi Msobi Mbelya ambaye aliumizwa wakati akipambana na wahalifu hao akiwa amelazwa hospitali ya Halmashauri ya Mji (Somanda) amesema kuwa baada ya watu kufika walimtishia kwa kusema akamatwe Kisha apigwe.

" Baada ya kusikia wakisema hivyo, nilianza kukimbia, ndipo nilipoanguka kwenye mtaro, baadaye nikasikia wanaanza kuvunja milango ya maduka kwa kutumia shoka" amesema Mbelya

Aidha Mlinzi huyo amesema Polisi walifanikiwa kufika haraka na kuanza kurushiana risasi, lakini baadaye Polisi walikimbia kurejea kituo Cha Polisi na waliporudi Mara ya pili walikuta majambazi hao wamekimbia.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni Joseph Mula alisema kuwa watu hao hawakufanikiwa kuiba kitu chochote na badala yake walifanya uhalibifu wa kuvunja maboksi ya kuhifadhia fedha pamoja na milango ya maduka.

Mula alisema kuwa Maduka yaliyovamiwa ni mawili yanayofanya Biashara ya miamala ya kifedha huku Duka la tatu likiwa linafanya Biashara ya kuuza Dawa Muhimu ambapo nako walivunja kofuli lakini hawakuingia ndani.

Naye Diwani kata ya Sima ambako tukio limetokea Zebedayo Kingi amesema kuwa wahalifu hao walifunga Barabara zote zinazoingia na kutoka kwenye maduka hayo.

" Tayari jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio hili, ni tukio baya ingawa hawakuchukua kitu, tunawaomba wananchi wawe watulivu, ingawa tunawashauri wenye maduka kutafuta walinzi wenye vifaa imara" alisema Zebedayo.

Wamiliki wa Maduka yaliyovamiwa wamesema kuwa baada ya kupata taarifa za uhalifu huo, walikimbia Moja kwa Moja kuja kwenye maduka na kukuta hakuna kitu kilichoibiwa.

" Nilifika Dukani nikakuta boski ya kuhifadhia fedha nilikiwa limebomolewa lakini walishindwa kulivunja kabisa, ndani kulikuwemo na Sh. Milioni tano, simu za miamala pamoja na mashine za Benki" Amesema Rebeca Masunga.

Naye Juda Sayi mmoja wa wamiliki wa Duka lilibomolewa, alisema kwenye dula lake hilo ni tukio la pili, ambapo miezi miwili iliyopita walifanikiwa kumwibia kiasi cha Sh. Milioni 24.

" Tunaomba ulinzi uhimalishwe kwenye huu Mji wa Bariadi, matukio yanaanza kuongezeka haya sasa, tunaomba serikali itusaidia maana tunashindwa kufanya Biashara" amesema Juda.

Hata hivyo mpaka Sasa jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu halijatoa taarifa yeyote juu ya tukio hilo, licha ya Kamanda wa Polisi kuombwa taarifa lakini hakujibu.

MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post