Mgombea Udiwani kata ya Bunamla kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkamba Zabron akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo, wakati wa uzinduzi wa Kampeini katika uchaguzi mdogo. |
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uzunduzi wa Kampeini uchaguzi mdogo kata ya Bunanhala, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. |
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uzunduzi wa Kampeini uchaguzi mdogo kata ya Bunanhala, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. |
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu leo kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Bunamhala ili kuziba nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo.
Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa
kata hiyo Samora Nhola Nsuzi aliyefariki Januari 24,2023 wakati akipatiwa
matibabu kwenye hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi.
Akizindua kampeni hizo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bariadi
Juliana Mahongo amesema nafasi inapokuwa wazi ni lazima uchaguzi ufanyike
kuiziba ili wananchi wapate mtu wa kuwasemea.
"Shughuli ambazo marehemu Samora Nhola Nsuzi alikuwa
amezianzisha na zingine ambazo zilikuwa bado zitaenda kumaliziwa na
Nkamba mpeni kura nyingine awatumikie wanabunamhala" Mahongo.
Kwa upande wake mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nkamba
Zabron amesema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo ataendeleza mambo mazuri
ambayo yameachwa na aliyekuwa diwani wa kata hiyo.
"Nitaendeleza yaliyoachwa na aliyekuwa diwani wetu na
mengine yanayokuja nipeni kura zenu niwatumikie nawahakikishia wanabunamhala
hamtajutia kura zenu" Zabron.
Awali mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bariadi Elias Masanja
amewaomba wanabunamhala kuchagua mtu sahihi wa kutatua changamoto zao.
"Wananchi wa Bunamhala naomba mridhie kwa moyo moja kwenda
kumchagua Nkamba Zabron akawatumikie Nkamba ataenda kuwawakilisha vema na
kutatua changamoto zenu kupitia Chama Cha Mapinduzi"Masanja
Aidha Masanja amesema majibu ya changamoto za wananchi wakiwemo
wa kata ya Bunamhala yapo kwenye Chama Cha Mapinduzi.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 13,2023 ili kumpata
diwani ambaye ataenda kuwawakilisha wananchi wa kata hiyo.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق