Mbunge Mayenga Awapiga Tafu ya Majiko ya Gesi Mama Lishe

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga ametoa msaada wa Majiko ya Gesi 250 kwa Mama Lishe Wilaya ya Kahama ili kuwarahishia kazi katika shughuli zao sambamba na utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala.

Mhe. Mayenga maarufu kwa jina la 'Dada Mkubwa' ametoa Majiko ya Gesi leo Jumatano Julai 5,2023 wakati wa Mkutano wake na Mama Lishe hao katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi majiko hayo, Mhe. Mayenga amesema ametoa mitungi yenye gesi ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo kwa Wajasiriamali na Mama Lishe Wilayani Kahama pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanawake katika shughuli za kiuchumi sambamba na kutunza mazingira kwa kutumia nishati mbadala.

“Nimetoa majiko ya gesi 250 kwa Mama Lishe wilayani Kahama na mengine 150 Wilaya ya Shinyanga hivyo kufanya idadi ya majiko kuwa 400 yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 20 ikiwa ni mwendelezo wa kuwasaidia mama lishe na Malengo ni kuwafikia mama lishe 800 mkoa mzima ili kuwarahishia akina mama kuepukana na majiko yasiyo rafiki kwa afya lakini pia kuepuka uharibifu wa mazingira. Lengo jingine ni kuwapunguzia gharama za kununua mkaa na nishati zingine”,amesema Mhe. Mayenga.
Muonekano wa sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa Mama Lishe wilayani Kahama

Katika hatua nyingine Mhe. Mayenga amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali anazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi hivyo kuwaomba Watanzania kuwapuuza baadhi ya watu wanaomsema vibaya Mhe. Rais Samia.

“Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika nchi hii. Zawadi pekee ya kumpa ni kumsema vizuri na kumsemea mema ilia pate moyo wa kuendelea kufanya kazi vizuri zaidi”,amesema Mhe. Mayenga.

Mbunge huyo wa Viti Maalumu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kutimiza wajibu wao wa malezi katika familia ili kuepukana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika jamii ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu katika familia.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amempongeza Mhe. Lucy Mayenga kwa kazi nzuri anayofanya katika kumkwamua mtoto wa kike, kupigania wanawake na wananchi kwa ujumla.

“Siku zote nasema Mpeni mtu maua yake akiwa hai. Mhe. Lucy Mayenga (Dada Mkubwa) ni jembe. Kitendo cha kugawa majiko kwa mama lishe ni kitendo cha kuigwa, hakuna ubaya kujifunza mambo mazuri kwa mwenzio”,amesema Mhe. Mhita.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akifurahia jambo.

Aidha Mhe. Mhita amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa fedha nyingi anazoendelea kuzileta wilayani Kahama kwa ajili ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu na ameendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Kahama Mhe. Theresphora Saria mbali na kumshukuru na kumpongeza Mhe. Lucy Mayenga kwa kuwapatia majiko ya gesi mama lishe wilayani Kahama, ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake kupendana,kushikamana, kushirikiana na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi kweny chaguzi mbalimbali.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Mhe. Grace Samwel Bizulu na Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Asha Juma Kitandala wamesisitiza umoja na mshikamano ndani ya chama ili kukijenga chama hicho.

Katika Mkutano huo pia UWT Wilaya ya Kahama imempatia zawadi Mhe. Lucy Mayenga kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kuu la UWT taifa.

 Lakini pia Benki ya Azania imetoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Mwanamke Hodari).

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na Mama Lishe na Wajasiriamali wilayani Kahama leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambapo pia ametoa msaada wa majiko 250 ya gesi kwa Mama Lishe wilayani humo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na Mama Lishe na Wajasiriamali wilayani Kahama leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiteta jambo na  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kulia).
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akiangalia majiko 250 ya gesi kabla ya kuyakabidhi kwa Mama Lishe wilayani Kahama.
Muonekano wa sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Muonekano wa sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa UWT Wilaya ya Kahama baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kuu la UWT taifa

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili kushoto) akionesha  zawadi kutoka kwa UWT Wilaya ya Kahama baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kuu la UWT taifa
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (aliyeshikilia ua) akipokelewa kwa shangwe baada ya kuwasili Wilayani Kahama

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (katikati) akipokelewa kwa shangwe baada ya kuwasili Wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (katikati) akicheza na mama lishe Wilayani Kahama

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Asha Juma Kitandala 
akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Kahama Mhe. Theresphora Saria akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Mhe. Grace Samwel Bizulu akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Mwanamke Hodari)

Mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama ukiendelea

Mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe wilayani Kahama ukiendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم