Mwenge wazindua mradi wa Maji Milioni 300 Itilima.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdalla Kaim akimtwisha ndoo yenye maji, mmoja wa akina mama katika kijiji cha Mwanunui Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu, baada ya Mwenge kuzindua mradi wa Maji katika kijiji hicho.

Na Derick Milton.

Wakazi zaidi ya 3000 wa Kijiji Cha Mwanunui Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, ni rasmi sasa wameondokana na adha ya kusaka maji umbali mrefu zaidi ya Kilometa 10 baada ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023 kuzindua mradi Mkubwa wa Maji kijijini hapo.


Mradi huo umezinduliwa leo, na Kiongozi wa Mbio hizo Mwenge Mwaka huu, Abdalla Kaim, ambapo amepongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kusimamia vyema mradi hadi kukamilika kwake.


Mradi huo ambao umetekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umegharimu kiasi Cha Sh. Milioni 300 fedha za serikali.


Mbunge wa Jimbo hilo Njalu Silanga Mara baada ya Mwenge kuzindua mradi huo, amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo hadi kukamilika na kueleza kuwa sasa wananchi wa Kijiji hicho watapata maji safi na salama.


Source. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم