Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
TIMU ya Ndoleleji Fc kutoka wilaya ya Itilima imenyakua Ubingwa wa Njalu Cup kwa kutwaa kikombe, fedha taslimu kiasi cha shilingi mil. 1 pamoja na medali za dhahabu baada ya kuigaragaraza Tetemeko FC kwa kuifunga goli 2-1.
Kombe la Njalu, limekuwa likiandaliwa kila mwaka na Mbunge wa Jimbo hilo Njalu Daud Silanga na kuzikutanisha timu kutoka kila kijiji ndani ya Jimbo hilo wilayani Itilima.
Mgeni Rasmi katika Mshindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Itilima Faidha Salim alimpongeza Mbunge huyo kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yamekuza vipaji na kufungua fursa ya ajira kupitia michezo kwa vijana.
Mkuu huyo wa wilaya alisema hivi karibuni, ataanzisha na kudhamini mashindano ya mpira wa pete na yatafanyika wilayani humo kwa kuzikutanisha timu mbalimbali kutoka mikoa jirani.
‘’Jiandaeni, nitadhamini mashindao ya mpira wa pete hapa Itilima…andaeni timu kutoka mikoa jirani, zawadi ya mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu nitatoa mwenyewe na kilele kitafanyika hapahapa’’ alisema Faidha.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Daud Nyalamu alimpongeza Mbunge huyo kwa ubunifu wa kuanzisha Mashindano ya Mpira wa miguu kupitia Njalu Cup.
Alisema Mbunge huyo amemhakikishia kuwa mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka ili kuwajengea uwezo vijana kuendelea kimichezo kwa kuonyesha vipaji kupitia mpira wa miguu.
Kocha wa Ndoleleji Fc, Asanteni Mwakalwanga alisema mashindao hayo ni mazuri sababu yanaibua vipaji kwa vijana na kila mwaka timu zinazidi kuboreka na vipaji vya vijana vinazidi kuonekana.
Bahati Kaluli, Kocha wa Tetemeko Fc alisema wamepoteza mchezo huo kutokana na vijana wake kufanya makosa madogmadogo na kuimboa ofisi ya Mbunge na Mkuu wa wilaya kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuibua soka na vipaji vya vijana.
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Faidha Salim akizungumza mara kwenye mashindano ya Fainali Kombe la Njalu liliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Lagangabilili.
Post a Comment