Na Derick Milton Simiyu.
|
|
|||
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, limetoa ufafanuzi wa taarifa zilizosambaa mapema leo Asubuhi katika mitandao ya kijamii kuhusu maafisa wa serikali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Simiyu, kudaiwa kupora fedha kwa kutumia siraha.
Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa Edith
Swebe amesema kuwa mara baada ya kupata taarifa hizo, wamefanya uchunguzi na
kubaini kuwa hakuna tukio la unyanganyi kwa kutumia siraha kama ambavyo
imeripotiwa.
Swebe amesema kuwa ni kweli maafisa hao walikuwa na gari hilo,
lakini hawakufanya tukio hilo bali walikuwa kwenye opereisheni za kawaida za
kutembelea vyama vya msingi vya ushirika kwa ajili ya kuangalia zoezi la
ununuzi wa pamba linavyoendelea.
Amesema kuwa wamechunguza na kubaini kuwa maafisa hao walikuwa
na ruhusa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya opereisheni hiyo, ambapo
ameeleza kilichoripotiwa hakikuwa sahihi.
“ Baada ya kupata hizo taarifa kupitia mitandao ya kijamii,
tukaanza uchunguzi wa haraka, naomba nitoe ufafanuzi hapa kuwa ndani ya mkoa wa
Simiyu na hasa Wilaya ya Maswa ambayo imetajwa hakuna tukio hilo,” amesema
Swebe.
“ Ni kweli gari ambalo limetajwa lilikuwa linafanya kazi zake za
opereisheni ya kawaida likitumiwa na maafisa hao kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
na hao watumishi waliotajwa walipewa ruhusa kwenda kufanya kazi hiyo,” amesema
ACP Swebe.
Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa “ yawezekana Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Maswa haikuwa na taarifa juu ya Opereisheni hiyo, na hata wananchi
hawakuwa na taarifa ndiyo maana ikazua taharuki”
Mapema Asubuhi ya leo katika mitandao ya kijamii ilidaiwa kuwa maafisa hao walifanya uhalifu huo kwenye vyama vya msingi vya Ushirika Wilayani Maswa wakiwa na gari la serikali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu DFP 9182.
Maafisa hao ilidaiwa walipora kiasi cha Sh. Milioni mbili katika Amcos ya Mwasita baada ya kumtishia kwa siraha katibu wa Amcos hiyo, pia wakapora Sh. 500,000 (Laki tano) kutoka Amcos ya Mwadila.
Ilidaiwa kuwa wakiwa katika harakati za kufanya halifu huo kwenye Amcos ya Mwamitumai, Maafisa hao walikurupushwa na Kamati ya Ulinzi na Usama Wilaya ya Maswa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Aswege Kaminyoge.
Hata hivyo hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alinukuliwa kudhibitisha uwepo wa tukio hilo, huku akimtaja mmoja wa maafisa hao (jina linahifadhiwa) kuwa amekamatwa na uchunguzi unaendelea.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق