Watu watatu wakamatwa kwa kuuwa Swala 28.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

 

JESHI la Polisi Mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Jeshi la Uhifadhi limefanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na nyara za serikali ambazo ni wanyamapori aina ya swala ishirini na nane.

 

Akitoa taarifa leo, august 18, mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe alisema operesheni hiyo imefanyika katika kijiji cha Mwasilimbi kata ya Ihusi wilayani Bariadi.

 

Kamanda Swebe amesema operesheni hiyo ilifanyika Agost 17, mwaka huu katika kijiji cha Mwasilimbi ambapo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na nyara za serikali.

 

‘’Watuhumiwa hao walikutwa na nyara za serikali, nyara hizo ni swala 28 aina ya Thomson wakiwa wameuwawa katika nyumba Musa Masunga,…tulikamata pia pikipiki moja aina ya Kinglion nyekundu yenye namba za usajili T. 874 CUA iliyokuwa ikitumika kuwatoa wanyamapori katika hifadhi yetu na kuwaleta katika makazi yao’’ amesema Kamanda Swebe.

 
Amewataja waliokamatwa kuwa ni Musa Madede (58), Musa Masunga (28) na Yunis Makwaya (45) ambaye ni mwanamke na wote wasukuma wakulima wa kijiji cha Mwasilimbi ambapo watuhumiwa pamoja na vielelezo watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 
 
Kwa upande wake Kamanda wa Pori la Akiba la Maswa, Afisa Mhifadhi Lawrence Okode amesema wamefanya opresheni hiyo imefanikiwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ambapo walifanikiwa kukamata watuhumiwa wakiwa wameuwa wanyama 28.

 

Amesema serikali imepata hasara ya milioni 38, lakini pia wamepoteza wanyama hao kwa maslahi ya watu binafsi na kwamba wanyama hao wanalindwa kwa mujibu wa sheria na maslahi ya watanzania wote.

 
MWISHO.
 
 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe akiwa na maofisa wa Jeshi la Uhifadhi, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kukamata watu watatu kwa tuhuma za kuuwa swala 28.
 
 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kukamata watu watatu kwa tuhuma za kuuwa swala 28.

Kamanda wa Pori la Akiba la Maswa, Afisa Mhifadhi Lawrence Okode akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya jeshi la polisi kutoa taarifa ya kukamata watu watatu kwa tuhuma za kuuwa swala 28.
 
 

 
 
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post