Bil. 250 zatekeleza miradi Maendeleo Simiyu.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akiongea na Waandishi wa Habari wa Mkoa humo hivi karibuni.
 


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

 

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Bil 250 ndani ya miaka miwili katika Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara.

 

Utekelezaji wa miradi hiyo umegusa kila kijiji, mitaa na vitongoji kwa lengo la kuwanufaisha wananchi na kuwaletea maendeleo na kuwasogezea huduma muhimu za kijamii.

 

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa huo Dk. Yahaya Nawanda wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

 

Amesema mkoa huo unaendelea kumshukuru Rais Samia kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kwenye kila kijiji, mitaa na vitongoji amewagusa na kuna miradi ya umeme, maji, elimu, afya au barabara inatekelezwa

 

‘’katika hizo Bil 250, sekta ya afya imepokea bil. 22.7, elimu bil. 27 kwenye elimu bure, ujenzi wa vyumba vya madarasa, thamani na vitabu…Wakala wa Barabara (TANROAD) Bil. 44, TANESCO Bil. 29 na katika vijiji 470 hakuna kijiji ambacho hakina umeme’’ amesema Dk. Nawanda.

 

Amefafanua kuwa hadi sasa vijiji vyote vya Mkoa wa Simiyu vina umeme, ambapo aliwataka wananchi kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kwani kabla ya miaka miwili vijiji asilimia 79 vijiji havikuwa na umeme.

 

Anaeleza kuwa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) wameshapokea Bil. 35 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara mbalimbali na kwamba mkoa huo umeshatengeneza barabara zenye urefu wa kilometa 700 ambazo hazikuwepo kabisa.

 

Ameongeza kuwa ufunguzi wa barabara kwenye zaidi ya kilometa 700 mkoani humo kutafungua mawasiliano kwa wananchi ikiwemo kuimarisha usafiri, usafirishaji na kurahisisha upatikanaji wa biadhaa na huduma kwa wananchi.

 

Katika hatua nyingine, Dkt. Nawanda amesema Mkoa huo umeanza kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/23 wamekusanya kwa asilimia 95.6 ya mapato yote na malengo ya mwaka huu kukusanya kwa asilimia 100.

 

‘’kwenye sekta ya elimu, katika hizo fedha, Rais ametupa Bil. 6.4 fedha kwa ajili ya kutekeleza pia ujenzi wa VETA, na tunamwomba akija atuzindulie chuo chetu…ufaulu umeongezeka, kwenye afya kuna mapinduzi makubwa sana na tumeletewa Bil. 8 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba ikiwemo CT Scan mashine mpya kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa’’ amesema Dkt. Nawanda.

 

MWISHO.

 

Waandishi wa Habari Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Dk. Yahaya Nawanda alipowatembelea ofisini kwao mjini Bariadi juzi, Sept 5, 2023.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (kulia) akiongea na waandishi wa Habari, kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo Frank Kasamwa.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (mwenye kofia katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari wa mkoa huo alipowatembelea ofisini kwao mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akitabasamu mara baada ya kuagana na waandishi wa habari alipowatembelea ofisini kwao juzi, sept 5, 2023.
 
 
 
 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post