Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Ismail Nawanda amewaagiza Wakuu wa Wilaya Mkoani Simiyu kuendelea kusimamia utekelezaji wa Shughuli za Usafi wa Mazingira kila mwisho wa Mwezi ili kuimarisha Usafi wa Mazingira Mkoani humo.
Dkt. Nawanda ameyasema hayo leo wakati akiwaongoza Wananchi na Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali Mkoani humo kufanya Usafi wa Mazingira katika eneo la Hospitali ya Wilaya iliyoko Somanda Halmashauri ya Mji Bariadi katika kuadhimisha siku ya Usafi wa Mazingira Duniani.
Amewataka Wananchi kuendeleza utamaduni wa kufanya Usafi wa Mazingira kila mwisho wa wiki ili kuweka Mji katika hali ya Usafi.
"Maeneo mengine wamefanikiwa kuweka miji yao katika Hali ya Usafi hivyo ni muhimu na sisi mkoa wa Simiyu kuiga mifano mizuri katika maeneo mengine kwa kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi Ili kuweka Mkoa wetu katika hali ya Usafi" Amesema Dkt. Nawanda.
Aidha Dkt. Nawanda amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bariadi kuhakikisha Usafi wa vyoo katika Stendi ya Mkoa wa Simiyu (Somanda) unafanyika Kila siku.
Mwisho.
Post a Comment