Kampuni ya Nyumbafasta inaleta suluhisho la kidijitali kwa wapangaji na wenye nyumba nchini Tanzania. Suluhisho hili litawawezesha wapangaji kupata nyumba za kupanga bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja na kuwasiliana moja kwa moja na wenye nyumba kwa gharama ndogo, kuanzia shilingi elfu moja tu.
Zaidi ya hayo, Nyumbafasta inawasaidia wanunuzi na wauzaji wa nyumba na viwanja kwa kutoa huduma ya uhakiki wa mali kupitia mfumo maalum. Mfumo huu umetengenezwa na vijana wa Kitanzania na unapatikana mtandaoni kote nchini kupitia tovuti yetu - www.nyumbafasta.co.tz.
Kupitia Nyumbafasta, wapangaji wanaweza kupata nyumba bora kwa bei nafuu na kusaidiwa kuokoa muda wa kutafuta nyumba, huku ikipunguza migogoro isiyo ya lazima wakati wa kununua nyumba au viwanja.
Tunawaalika wamiliki wa nyumba za kupangisha nchini kote kujisajili kwenye tovuti yetu bila malipo yoyote kupitia www.nyumbafasta.co.tz au kutumia huduma bora na yenye uweledi isiyo na gharama kupitia kitengo chetu cha huduma kwa wateja.
Tunawakaribisha kutumia Nyumbafasta kwa huduma ya upangaji bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja na ununuzi wa nyumba na viwanja vilivyo hakikiwa ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Pamoja na hayo tumechukua hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wetu na jamii na kuendeleza huduma bora kwa wateja wetu.Tunayo furaha kumkaribisha Barbara Hassan katika jukumu hili muhimu la kuwa mwakilishi wetu mpya na balozi wa kampuni yetu. Hii yote ni
katika kuhakikisha tunabaki kuwa kinara katika sekta ya uuzaji na upangaji wa nyumba na viwanja. Tunayo furaha kubwa kutangaza uteuzi huu wa Balozi Mpya katika timu yetu,
Barbara Hassan - tukiamini katika uchapaji wake kazi. Barbara amepata sifa kubwa katika sekta ya utangazaji kutokana na uzoefu wake mkubwa na uwezo wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika jamii.
Tunaamini Barbara atachangia maarifa na utaalamu wake kuhakikisha tunabaki kuwa chaguo la kwanza na bora kwa wateja wetu na kuendeleza miradi yetu ya upatikanaji wa Nyumba na Viwanja kwa haraka.
Ameonesha dhamira ya dhati katika kuendeleza sekta ya Nyumba za kupanga, Nyumba za kuuza na Viwanja kwa kutoa huduma bora kwa wateja. Tunatarajia kufanya kazi kwa karibu naye ili kuleta mafanikio makubwa kwa kampuni yetu.
Kampuni yetu - Nyumbafasta - inajitolea kuendelea kuwa wabunifu na kutoa huduma za hali ya juu katika sekta hii. Uteuzi wa Balozi Mpya ni hatua muhimu katika kufanikisha malengo haya yanatimia.
Tunasema Makato yasio ya lazima Sio Shida Zetu
Kwa maelezo zaidi au kwa mahojiano, tafadhali wasiliana na: Robinson Marley 0652493300.
إرسال تعليق