Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda akizungumza na walimu
mbalimbali wa mkoa huo (hawapo pichani) wakati wa Warsha ya siku moja ya
Mwalimu Spesho iliyoandaliwa na Benki ya NMB. |
Na Derick Milton Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda amewataka wakurugenzi wote na Maafisa Utumishi katika Halmashauri zote za Mkoa huo, kuhakikisha wanawasimamia walimu ipasavyo ili wasijiingize katika mikopo umiza.
Dkt. Nawamda amesema kuwa walimu wengi wameendelea kuteseka na taasisi ambazo siyo rasmi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo, huku baadhi yao wakiamua kuacha kazi kutoka na kukubwa na madeni mengi na makubwa.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maagizo hayo leo, wakati akifungua warsha ya siku ya moja ya Siku ya Mwalimu Mkoani humo ijulikanayo kama Mwalimu Spesho ambayo iliandaliwa na Benki ya NMB.
Amesema kuwa Maafisa Utumishi wanatakiwa kuwa walezi na washauri wa walimu mara kwa mara, pindi Mwalimu anapohitaji kukopa kwa kumpeleka katika taasisi ambazo zinatambulika kisheria.
“ Ninazo kesi nyingi za walimu wamekopa kwenye taasisi ambazo siyo rasmi, na wamefilisiwa, mmoja wa Mwalimu alikopeshwa Milioni mbili akakatwa riba ya Milioni 72, walimu wengi wamefilisiwa,” amesema Dkt. Nawanda.
Dkt. Nawanda ameeleza kuwa wapo Maafisa utumishi wengine wamekuwa madalali wa taasisi hizo ambazo siyo rasmi, ambapo wamesababisha walimu kukopa kisha kufilisiwa na kuacha kazi.
“ Mwalimu anakopa hadi asilimia 100 ya mshahara wake, alafu wewe Afisa Utumishi upo ofisini na unaona, tunajua baadhi yenu mnahusika, nichukue nafasi hii kuwaonya, ukibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yako,” ameongeza Dkt. Nawanda.
Katika Hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka na walimu kubadilika na kwenda katika taasisi ambazo ni rasmi ikiwemo benki ya NMB kwa ajili ya kupata mikopo yenye riba nafuu.
“ Hata sisi walimu tubadilike sasa, tuache kwenda kwenye hiyo mikopo umiza, NMB leo wamekuja na mikopo yenye riba nafuu kupitia kifurushi cha Mwalimu Spesho, tukitumia njia hii tutafanya kazi kwa amani,” amesema Dkt. Nawanda.
Nawanda ameipongeza NMB kwa kuona umuhimu wa kukutana na walimu na kuwapa elimu ya ujasliamali pamoja na kuwanoyesha huduma mbalimbali za mikopo inayotolewa na benki hiyo kupitia mfumo wa Mwalimu Spesho.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema kuwa kada ya ualimu bado imeendelea kukubwa na changamoto kubwa ya kwenda kukopa katika taasisi za kifedha ambazo siyo rasmi na baadaye kukubwa na msongo mkubwa wa mawazo kutokana na mikopo wanayopata kuwa na riba kubwa.
Amesema kuwa Benki ya NMB baada ya kuona changamoto hiyo, iliamua kuanzisha utaratibu wa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa kada hiyo kupitia mfumo wa Mwalimu Spesho ambayo inamwezesha Mwalimu kuondokana na mikopo umiza.
“ Wote tunajua kuwa kada ya ualimu ndiyo imeathirika zaidi na mikopo hii umiza, wengine wakiita kausha damu, Walimu wamekuwa wakipata mikopo hii kwa riba kubwa sana na kusababisha matatizo makubwa kwao ikiwemo msongo wa mawazo” amesema Urio.
Emmanuel Silivester mmoja wa walimu amesema kuwa Mikopo umiza imesababisha walimu wengi kuendelea kupata matatizo mbalimbali ikiwemo kukosa amani pindi wawapo kazini.
Silivester ameishukuru NMB kupitia huduma ya Mwalimu Spesho, ambayo ameeleza walimu itasaidia kuondokana na changamoto za kukosa amani kazini na kufilisiwa mali zao.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio, akizungumza
wakati wa warsha ya siku moja ya Mwalimu Spesho iliyowakutanisha walimu wa Mkoa
wa Simiyu, Warsha hiyo imeandaliwa na benki ya NMB. (wa kwanza kushoto) Meneja
Mwandamizi Mauzo NMB Isaac Mgwasa.
|
Meneja Mwandamizi Mauzo benki ya NMB Isaac Mgwasa akizungumza wakati wa warsha ya Mwalimu Spesho Mkoani Simiyu iliyoandaliwa na Benki hiyo, Warsha hiyo imelenga kuwaelimisha walimu fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
Meneja Mauzo NMB Kanda ya Magharibi Trifon Melkiory akizungumza na walimu wakati wa warsha ya siku ya Mwalimu Mkoani Simiyu iliyoandaliwa na Benki hiyo. |
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment