Walengwa wa TASAF sasa kulipwa fedha Taslimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete (kulia) akizungumzia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), unavyotekeleza miradi ya Maendeleo, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Mwanakhamis Kawega.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda ameipongeza serikali kwa kubadili mfumo wa malipo kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) ambao huko nyuma walikuwa wanapokea fedha kwa njia ya simu na benki.

 

Amesema kutokana na mfumo huo, baadhi ya walengwa walikuwa hawapati malipo kwa wakati jambo ambalo TASAF inahusisha wananchi wa hali ya chini sana ikiwemo wazee ambao hawana uwezo wa kutumia mifumo ya kibenki ikiwemo simu hali ambayo ilikuwa inasababisha changamoto ya kukosa malipo yao.

 

DK. Nawanda ameyasema hayo leo wakati akitoa akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete aliyefanya zaiara ya siku moja kwa ajili ya kuongea na watumishi wa umma pamoja na kukagua miradi ya TASAF.

 

aidha, amesema wananchi wanapata changamoto ya uchangiaji wa asilimia 10 ya miradi ya TASAF, jambo ambalo linakwamisha utekelezaji wa miradi kwa wakati kutokana na wananchi kukosa fedha au uhaba wa nguvu kazi.

 

Awali Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Nyasilu Ndulu amesema wanatekeleza miradi ya kuondoa umaskini awamu ya nne (TPRP IV) ambapo jumla ya shilingi Bil. 9.2 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu na kukuza uchumi wa kaya.

 

Amesema hadi sasa zaidi ya Bil. 6 zimetumika sawa na asilimia 65, jumla ya kondoo 2947 wenye thamani ya mil. 217.7 wamegawia vikundi 52, mbuzi 459 wenye thamani ya mil. 22.5 katika vikundi 12 na mil. 9.6 zimetumika kununua mizinga 150 na kupewa vikundi 12.

 

Amezitaja baadhi ya changamoto za utekelezaji wa miradi ya TASAF ni pamoja na kuchelewa kukamilisha utekelezaji wa miradi ya TI na PWP, kusuasua kwa michango itokanayo na nguvu za jamii, uwepo wa mvua nyingi, kutofuta kalenda ya malipo na walengwa kuhama bila kuujulisha uongozi.

 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete amesema ameridhishwa na Utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) huku wanufaika wake ni wananchi wasiokuwa na uwezo.

 

Amesema miradi ya TASAF ni tofauti na miradi mingine ya serikali kwa sababu inaonekana kwa macho na utekelezaji wake unawagusa wananchi waishio vijijini moja kwa moja.

 

‘’TASAF wana Uwezo wa kuzisimamia hizo fedha, kama hakuna uwezo wa kuzisimamia, tutaishia kugombana tu, tunachotaka tukileta fedha tuone thamani halisi ya fedha hizo…hivi ndivyo miradi inavyotakiwa kufanyika’’ amesema Ridhiwan.

 

Amezitaka Halmashauri kujifunza kwenye miradi ya TASAF ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na inatekelezwa na watu wanaotaka matokeo yanayooneka.

 

Amefafanua kuwa moja ya kundi kubwa linalonufaika na miradi ya TASAF ni kaya maskini ambazo hazina uwezo wa kulipia watoto mahitaji ya shule, uhakika wa kupata matibabu na chakula.

 

MWISHO.

 

Baadhi ya watendaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete (hayupo pichani).

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete (katikati), kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mwanakhamis Kawega.

 


Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Nyasilu Ndulu akiwasilisha taarifa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete (hayupo pichani).

 
 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akiongea namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) ulivyochochea maendeleo katika Mkoa huo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete alipotembelea mkoa huo leo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete (katikati), kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mwanakhamis Kawega.
 
 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post