Na Mwandishi wetu.
Jumla ya Watahiniwa 1,397,370 wa darasa la saba nchini, wataanza kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi kuanzia kesho Septemba 13 hadi 14, 2023.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed, na kusema kati ya watahiniwa hao, 654,652 ni wavulana wasichana ni 742,718.
Ambapo wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia mitihani, wasimamie mitihani kwa makini na uadilifu wa hali ya juu na wazingatie kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa ili kila mtahiniwa apate haki yake.
MWISHO.

إرسال تعليق