Mapacha wafariki wakiwaongezewa matiti kwa mganga wa kienyeji.

 


Na Derick Milton, Bariadi.

Watoto wawili wa kike ambao wote ni mapacha wenye umri wa miaka 17 wanaoishi katika kijiji cha Bubale kata ya Nkololo wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia kutokana na kile kinachodaiwa kupewa dawa ya kukuza matiti na mganga wa kienyeji.

 

Mganga huyo ambaye ni mkazi wa Byuna Wilayani humo aliyejulikana kwa jina la Masunga Tumolo alikuwa akiwapatia dawa hiyo ya kukuza matiti ili wapate kuolewa. 

 

Tukio hilo limetokea jana oktoba 04, 2023 katika kijiji cha Byuna ambapo ndipo anapoishi mganga huyo.

Wananchi wa kijiji hicho wameeleza kuwa watoto hao wamepoteza maisha katika nyakati tofauti.


Mganga mfawidhi kituo cha Afya Byuna Dkt. Deogratius Nteki amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza leo Septemba 05, 2023 majira ya saa 10:00 Alfajiri aliletwa mtoto mmoja kati ya hao katika kituo hicho.

 

“ Mtoto huyo alikuwa na hali mbaya, akitapika damu, tulimpatia huduma lakini alipoteza maisha, baadaye mwingine aliletwa naye akiwa katika hali mbaya, katika kumpatia matibabu naye alipoteza maisha,” amesema Dkt. Nteki.

 

Mganga Mfawidhi huyo amesmea kuwa chanzo cha kifo ni watoto hao kupewa dawa inayodhaniwa kuwa na sumu alipopelekwa kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

 

Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Simalenga ameagiza wahusika wote akiwemo Mganga huyo wa kienyeji, kusakwa popote walipo na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم