Na Mwandishi Wetu, Bariadi.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kujeruhi mwanae inayomkabili Askari wa Jeshi la Polisi H.4178 Abati Benedectio wa kituo Cha Polisi Bariadi.
Mashahidi wa upande wa jamhuri wa Kesi ya jinai namba 59/2023 inayomkabili mshitakiwa, wamemaliza kutoa ushahidi wao mahakama ya wilaya ya Bariadi na kinachosubiri ni kutolewa kwa uamuzi mdogo
Askari huyo anakabiliwa na mashtaka ya kumjeruhi moto wake mwenye umri wa Miaka saba Tukio linalotajwa kutokea January 15 mwaka 2023 akidaiwa kumuadhibu mtoto huyo baada ya kushindwa kusoma na kumsababishia majeraha maeneo mbalimali ya mwili wake
Shahidi namba 6 ni ASP. Gaudent ambae alikua mkuu wa upelelezi msaidizi wa wilaya ya Bariadi ambapo ametoa ushahidi wake mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bariadi Caroline Kiliwa ambapo ameieleza mahakama kua mnamo January 20, 2023 majira ya saa saba mchana alipokea maelekezo Toka Kwa mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Bariadi kufungua jalada kuhusu tuhuma za PC Abbat kumshambulia mtoto wake.
Alifungua jalada lenye namba BAR/CID/PE/01/2023 na alianza upelelezi Kwa kumtembelea mtoto Abbat Benedicto aliekua amelazwa katika hospital ya mji wa Bariadi ambapo alibaini mtoto huyo kua na majeraha sehemu za mgongoni, shingoni, na sikioni na alipomhoji mtoto alimweleza kua alipigwa Kwa fimbo na baba yake baada yakushindwa kusoma, kuandikia na kufanya hesabu
Shahidi namba 6 aliendelea kuieleza mahakama kua aliendelea na upelelezi Kwa kumhoji mtuhumiwa PC Abbat ambae alikiri kumuadhibu mtoto wake mnamo January 15/2023 Kwa kumchapa fimbo tano kwenye makalio na baadae mtoto aliangukia kwenye kochi na kupata jeraha sikioni na yeye alieondoka kwenda kumtafutia dawa mtoto wake
Shahidi namba 6 akaeleza kua baada ya uchunguzi alibaini kua mtoto huyo alifanyiwa ukatili kutokana na taarifa Toka Kwa mashahidi aliowahoji ambao walisema kweli mtoto alichapwa na baba yake na kuona Iko haja ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ndipo alipofungua jalada halisi la ukatili dhidi ya mtoto namba BAR/IR/274/2023 na kulipeleka ofisi ya Taifa ya mashtaka
Mwendesha mashtaka wa Serikali Francis Mbaga akamtaka shahidi namba 6 kutoa ufafanuzi juu ya jalada la upelelezi alilolifungua ambapo shahidi alifanunua kua jalada Hilo lenye namba BAR/CID/PE/01/2023 ni jalada maalum analofunguliwa mtumishi wa jeshi la Polisi anapotuhumiwa Kwa makosa yoyote ya kinidhamu
Hakimu mfawidhi Caroline Kiliwa alimpa nafasi mshitakiwa kumuuliza maswali shahidi ambapo miongoni mwa maswali aliyouliza ni pamoja na kama shahidi alimhoji mtoto kubaini kama ana changamoto nyingine ya kiafya ambapo shahidi alijibu kua alimhoji na alibaini kua mtoto changamoto ya upungufu wa damu
Shahidi alimaliza kutoa ushahidi wake kwa kumtambua mshitakiwa mahakamani hapo
Kesi hiyo imeahirishwa Hadi December 28/2023 ambapo mahakama itatoa uamuzi mdogo.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment