Makonda atua Simiyu, atawazwa jina la Bagolole.

MACHIFU wa Mkoa wa Simiyu wakimsimika Paul Makonda na kumpa jina la Bagolole kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa stendi ya zamani mjini Bariadi.

 

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

 

KATIBU wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amewasili Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 20 backo to back.

 

Akiwa Mkoani humo, Umoja wa Machifu wa kabila la Wasukuma wamemtawaza Makonda kwa jina la Bagolole ikimaanisha WANYOOSHE, huku akisema muda wa kuwanyoosha Wakandamizaji umefika.

 

Akizungumza leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya zamani Bariadi, Makonda amesema kilimo cha Mkoa wa Simiyu ni kilimo cha kujikumu na siyo kilimo cha kusubiri Amcos wawalipe wakulima.

 

‘’Maelekezo ya Chama, hawa wakina mama waachwe wauze sokoni kwa mteja wanayemtaka kumuuzia, nafahamu mpango wenu wa stakabadhi ghalani ni mwema lakini katika hili tupeni muda, kilimo kinahama kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kimataifa’’ amesema Makonda na kuongeza.

 

‘’Maafisa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, nendeni kwa wakulima, Chama kilishamwelekeza Waziri Bashe, Mnafahamu Rais Samia katoka pikipiki kwa watendaji wa kilimo nchi nzima, katoa pikipiki, ipad na vipimo vya udongo’’

 

Amewataka kumwamini na kumwombea Dk. Samia Suluhu Hassan, huku akisisitiza kuwa kuna baadhi ya watu wamepewa nafasi kwenye ofisi za umma na kwamba majibu wanayotoa siyo maelekezo ya Dk. Samia bali ni majibu yao.

 

MWISHO.
















 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم