WAJUMBE wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu wakimsimika Ungole Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu na kumpa jina la Ngole Sane.
Na Costantine Mathias, Bariadi.
BARAZA la Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu jana
(Januari 14, 2024), limemsimika Ungole Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo, Ester
Midimu na kumpatia jina la Sane kutokana na kuwatumikia Wanawake kwa muda
mrefu.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Mariam Manyangu
amesema wamemsimika Mbunge huyo wa Viti Maalumu kutokana na juhudi zake
anazozifanya ikiwemo kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali ikiwemo
huduma za Maji, Afya na Elimu.
Akitoa shukrani baada ya tukio hilo, Mbunge Ester
amewapongeza wanawake hao kwa kuendelea kushirikiana nae huku akiahidi kuendelea
kuwatumikia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kuwasilisha kero zao kwa Dk. Samia
Suluhu Hassan.
‘’Nitaendelea kuwatetea wanawake wa Mkoa wa Simiyu
na maeneo mengine ili mpate mahitaji msingi ya kibinadamu, nitahakikisha
mnapata haki sawa za kielimu, afya na huduma za maji’’ amesema Mbunge Ester.
MWISHO.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Mariamu Manyangu ( wa pili kulia) na Katibu wa UWT mkoa huo Modester Mwaya (wa kwanza kulia), kushoto ni Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Simiyu Lumeni Mathias.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu (mwenye kaniki nyekundu) akiongea na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Mkoa huo mara baada ya kusimikwa Ungole na kupewa jina la Ngole Sane.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Ester Midimu akiongea na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa huo ambao hawapo pichani, mara baada ya kusimikwa Ungole.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment