Na Derick Milton.
Mwaka 2023 Shirika la
Finscope linalojihusisha na masuala ya uboreshaji maisha, ustawi, na uwezeshaji
wa Watanzania kupitia ushirikishwaji wa kifedha, lilifanya utafiti wa masuala
mbalimbali ya kiuchumi.
Katika utafiti huo
uligusa mambo muhimu kwa wafanyabiashara na wajasliamali wadogo wadogo ikiwemo
nidhamu ya kifedha, uwekezaji pamoja na uwekeji akiba.
Utafiti huo unaonyesha
uwepo wa idadi kubwa watanzania ambao wapo kwenye myororo wa ufanyaji biashara
lakini hawana elimu juu ya masuala ya kifedha.
Katika eneo moja la
utafiti huo, linaonyesha kuwa kati ya watu 10 wenye akaunti Benki ni mtu mmoja
tu ndiye amekopa katika taasisi ambazo ni rasmi za kifedha.
Hali hiyo inaonyesha
dhahiri kuwa kuna idadi kubwa ya watu hasa wafanyabiashara na wajasliamali
wanakopa katika taasisi ambazo siyo rasmi na kupata madhara makubwa ya
kiuchumi.
Eneo la Elimu ya
kifedha linatajwa kuwa suruhisho pekee ambalo linaweza kumwinua mfanyabiashara
au mjasliamali mdogo mdogo kukua kiuchumi na kukuza biashara zake.
Benki kuu ya Tanzania
(BOT) katika miongozo yake, imeendelea kuzisisitiza taasisi mbalimbali za
kifedha ambazo ni rasmi, kuwekeza zaidi katika eneo la elimu ya kifedha kwa
watanzania.
Baadhi ya taasisi hizo
za kifedha zimekuwa zikitekeleza ipasavyo miongozo hiyo, ambapo elimu imekuwa
ikitolewa mara kwa mara pamoja na kuja na masuruhisho mbalimbali yanayoweza
kuwainua wananchi kiuchumi.
Benki ya NMB Tanzania
ni moja ya taasisi ambayo imeendelea kutekeleza miongozo hiyo kwa vitendo,
kwani imekuwa ikitoa elimu kupitia programu na kampeini mbalimbali
inayozianzisha kwa wateja wake.
Baadhi ya programu
hiyo ni Mwalimu Spesho ambayo utoa masuruhisho mbalimbali ya kifedha kwa
wakulimu, NMB Kikundi Akaunti ambayo ni maalumu kwa vikundi vya kijamii.
Programu nyingine ni
NMB Jiwekee inayowawezesha mteja weke walioko nje ya mifumo rasmi ya ajira
kujiwekea akiba, lakini pia program ya Mshiko Fasta ambapo mteja anaweza kupata
mkopo usiohitaji dhamana wala ujazazi fomu.
Licha ya Kampeni hizo
ambazo zina masuruhisho mbalimbali ya kifedha na kuwalenga zaidi wateja wake,
NMB imekuja na kampeini mpya inayolenga kutoa elimu ya kifedha hasa kwa makundi
ya vijana na wanawake.
Kampeni hiyo imepewa
jina la NMB Nondo za Pesa ambayo imezinduliwa wiki hii Jijini Dar es Salaam
ambapo itatekelezwa na Benki hiyo ichi nzima kupitia makongamano mbalimbali
pamoja na kuhasishwa kupitia vyombo vya habari.
Filbert Mponzi ni
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB akimwakilisha Afisa Mtendaji
Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna wakati wa uzinduzi wa Kampeini hiyo..
Anasema kuwa NMB
imekuja na programu hiyo ili kuongeza uelewa wa masuala ya kifedha kwa
maendeleo na ukuaji uchumi kwa Mtanzania mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Anasema kuwa Programu
hiyo ya kifedha ni endelevu ambapo walengwa ni watanzania wote, lakini kwa
upekee, ikiwa na vipengele maalumu vinavyowagusa zaidi na Vijana na Wanawake.
Anasema kuwa kupitia
NMB Nondo za Pesa, benki hiyo itakuwa inatoa elimu kwenye mada muhimu zote
kuhusiana na fedha, ikiwamo namna ya kupanga bajeti, kuweka akiba, uwekezaji,
mikopo, bima na mipango mingine ya kifedha.
“ Tunajua asilimia 66
ya watanzania ni vijana, NMB tunaona kundi hili ni muhimu sana na kwa asilimia
kubwa lipo katika mnyororo mkubwa wa biashara, lakini linapokuja suala la
kukuza uchumi mtu wa kwanza kuangaliwa ni mwanamke,” anasema…
“ Hata kwenye familia
zetu mwanamke ndiyo nguzo kuu ya uchumi wa familia zilizonyingi, kutokana na
makundi hayo kuwa muhimu, programu hii imekuja na vipengele maalumu katika kutoa
elimu ya kifedha kwao,” anasema Mponzi.
Katika eneo la kuweka
Akiba Afisa huyo wa NMB anasema kuwa bado watanzania wapo nyuma kwenye eneo
hilo, ambapo benki hiyo imeona umuhimu wa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali
kujiwekea akiba.
“ Unakuta mfanyabiashara
anafanya kazi yake lakini hana mpango wa kujiwekea akiba kwa ajili ya kumsaidia
baadaye katika mazingira yeyote, NMB kupitia programu hii tumeona hiyo ni
changamoto lazima elimu itolewe,” anaeleza Mponzi.
Aidha katika eneo la
uwezekezaji, Programu hiyo anasema imelenga kuwapa elimu wale ambao hajui fursa
za uwekezaji zinapatikana wapi na unaweza kuwekeza vipi na kiasi gani cha pesa
uwekeze.
“ Kuna watu wanazo
pesa zao au wamekuwa wakipata pesa, lakini hawajui wapi wawezeke pesa hizo,
kupitia NMB Nondo za Pesa, tumekuja na suruhisho la kuwaonyesha wale wenye nia
ya kuwekeza wapi wawekeze lakini na kuwapa elimu ya umuhimu wa kuwekeza.
Hata hivyo NMB bado
hajaliacha nyumba tatizo la mikopo umiza au mikopo kausha damu ambayo
imeendelea kuwakumba wafanyabiashara au wajasliamali wadogo wadogo nchini.
Kampeini hii eneo la
mikopo haijaliacha nyuma, kwani elimu itatolewa kwa makundi mbalimbali hasa
vijana na wanawake ambao ndiyo wahanga wakubwa wa mikopo umiza na kausha damu.
Mponzi ana
ainabainisha kuwa wengi ambao wamekuwa wakikubwa na mikopo umiza na kausha
damu, hawana elimu ya sehemu gani sahihi wanaweza kupata mikopo kwa haraka,
riba nafuu na inayoendana na biashara zao.
Anabainisha kuwa
kukosekana kwa elimu hiyo, wengi wamejikuta wanakimbilia katika taasisi ambazo
siyo rasmi na kujikuta wamejiunga katika mikopo ya taasisi hizo ambayo mwisho
wake unakuwa mbaya.
“ NMB Nondo za Pesa
imekuja na masuruhisho ya changamoto hiyo, tutatoa elimu ya umuhimu wa kukopa
katika taasisi rasmi, lakini tutawaonyesha mikopo inayopatikana NMB tena yenye
riba nafuu na inayopatikana kwa haraka,” anaeleza Mponzi…
Frank Silvester Mrope
ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki na Bajaji
(CMPD) Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam anasema kuwa ujio wa NMB Nondo
za Pesa ni dawa tosha ya kutibu matatizo ya kifedha waliyonayo.
“NMB wamekuwa wadau
wetu wakubwa, wametukopesha pesa, lakini pia vyombo vya usafiri kama pikipiki
na bajaj, kwa hiyo sisi ni wanufaika wakubwa wa huduma zao na walichofanya hapa
ni kutuongezea elimu zaidi za utafutaji na uwekaji akiba kwa faida yetu na
vizazi vyetu,” anasema Mrope.
Anatoa wito kwa
bodaboda na bajaji wenzake ambao wako nje ya vyama, wajitokeze kujisajili ili
kuingia kwenye mifumo rasmi ya kibenki, waweze kukopesheka, kwa sababu ni ngumu
kwao kupata fursa wakiwa nje ya mifumo.
Naye Ruth Lema
Mjasliamali wa Soko la Mbezi kwa Beda, anasema kuwa uzinduzi wa NMB Nondo za
Pesa umekuja na manufaa makubwa kwao kwani wamejifunza vitu vingi ikiwemo fursa
za ukopaji, uwekezaji, bima na masuala mazima ya elimu ya fedha.
“Tumefurahia uzinduzi
huu, umetuongezea vitu vingi ikiwemo namna mbalimbali za kukopa, matumizi
sahihi na umuhimu wa urejeshaji wa mikopo na fursa zingine nyingi kwa vijana na
wanawake. Wito wangu kwa wajasi;iamali wote kujiunga na vikundi vya kijamii na
kunufaika pamoja na huduma za NMB,” anasema Bi. Ruth.
MWISHO.
Post a Comment