TCB yafichua siri kitalu cha Mbegu ya Pamba kuhamishwa Mwabusalu.

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini (TCB), Marco Mtunga akizungumza katika mkutano wa kujadili uzalishaji na ununuzi wa Pamba Mkoani Simiyu.

 

Na Costantine Mathias.

 

MKURUGENZI wa Bodi ya Pamba nchini (TCB), Marco Mtunga amefichua siri ya kitalu cha kuzalisha mbegu ya Pamba cha Mwabusalu wilayani Meatu Mkoani Simiyu kuhamishwa na kupelekwa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ilitokana na wataalamu Kutoka Ukirigulu kutishiwa na Viongozi wa vijijii kukatwakatwa mapanga wakipinga ukataji wa masalia ya Pamba.

 

Mtunga amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali ikiwemo kuchanganya mahindi na pamba jambo ambalo limekuwa likiwasabibishia tija ndogo wakulima.

 

Akizungumza jana kwenye kikao kilichokutanisha Wanunuzi wa Pamba, Viongozi wa Chama kikuu cha Ushirika (Simcu), viongozi wa Amcos, wakulima, watendaji wa vijiji na mitaa, ambapo amesema wakulima wa Pamba wa Mkoa wa Simiyu wanahitaji maendeleo bila maarifa ambapo utaalamu au Sayansi ya Kilimo inapigwa vita.

 

Mtunga amesema wakulima wa Pamba wa Mkoa wa Simiyu wanahitaji maendeleo bila maarifa ambapo utaalamu au Sayansi ya Kilimo inapigwa vita.

 

‘’Pamba ya mwaka jana ikilala, ukachanganya na pamba ya mwaka huu utabeba wadudu wote wa mwaka jana kupeleka msimu mpya…wote mmeona masalia ya pamba wakati viongozi wenye nafasi tupo, maana yake kila mtu anapuuza Sayansi’’ amasema Mtunga.

 

MWISHO.

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga katika kikao cha kujadili Uzalishaji na ununuzi wa Pamba mkoani humo.


Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu Lumeni Mathias (kulia) akiwa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo katika mkutano wa kujadili uzalishaji na ununuzi wa zalo la Pamba uliofanyika ukumbi wa shule ya sekondari Kusekwa Memorial.




Watendaji wa kata pamoja na viongozi wa Amcos wakiwa katika mkutano wa kujadili uzalishaji na ununuzi wa zao la Pamba mkoani Simiyu.




 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post