Na Costantine Mathias.
MKURUGENZI wa Bodi ya Pamba nchini (TCB), Marco Mtunga amefichua siri ya kitalu cha kuzalisha mbegu ya Pamba cha Mwabusalu wilayani Meatu Mkoani Simiyu kuhamishwa na kupelekwa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ilitokana na wataalamu Kutoka Ukirigulu kutishiwa na Viongozi wa vijijii kukatwakatwa mapanga wakipinga ukataji wa masalia ya Pamba.
Mtunga amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali ikiwemo kuchanganya mahindi na pamba jambo ambalo limekuwa likiwasabibishia tija ndogo wakulima.
Akizungumza jana kwenye kikao kilichokutanisha Wanunuzi wa Pamba, Viongozi wa Chama kikuu cha Ushirika (Simcu), viongozi wa Amcos, wakulima, watendaji wa vijiji na mitaa, ambapo amesema wakulima wa Pamba wa Mkoa wa Simiyu wanahitaji maendeleo bila maarifa ambapo utaalamu au Sayansi ya Kilimo inapigwa vita.
Mtunga amesema wakulima wa Pamba wa Mkoa wa Simiyu wanahitaji maendeleo bila maarifa ambapo utaalamu au Sayansi ya Kilimo inapigwa vita.
‘’Pamba ya mwaka jana ikilala, ukachanganya na pamba ya mwaka huu utabeba wadudu wote wa mwaka jana kupeleka msimu mpya…wote mmeona masalia ya pamba wakati viongozi wenye nafasi tupo, maana yake kila mtu anapuuza Sayansi’’ amasema Mtunga.
MWISHO.
إرسال تعليق