CCM yapokea Wanachama wapya 100 Busega

Wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM) kata ya Nyaruhande wilayani Busega.

 

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea Wananchama wapya 100 kutoka kata ya Nyaruhande wilayani Busega Mkoani Simiyu baada ya kuridhisha na Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo unaofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

 

Wakizungumza jana mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Uanachama kwenye Maadhimisho miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika kata hiyo, wanachama hao wapya wamemshukuru Dk. Samia pamoja na wasaidizi wake kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara.

 

Scolastika Manyanda, mkazi wa Nyaluhande alisema serikali ya CCM inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inaleta tija kwa wananchi, hivyo hawana budi kuunga mkono jitihada hizo.

 

‘’tumeamua kujiunga na CCM kwa hiari yetu wenyewe kwa sababu tunaona jitihada zinazofanywa…hatukuwa na wanachama wa chama chochote, tunaipongeza serikali kwa miradi ya Maji, Elimu, Afya, Barabara na Umeme ambao umefika mpaka vijijini’’ alisema Scolastika.

 

Awali katibu wa CCM wilaya ya Busega Steven Koyo alisema Chama hicho kimepokea wanachama wapya 50 waliopatiwa kadi za CCM pamoja na vijana wengine 50 waliopatiwa kadi za Umoja wa Vijana (UVCCM).

 

Aliwataka wanachama hao kuendelea kuiamini CCM, chama ambacho kinaongoza dola na kwamba kinaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani akati huo miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa kila mahali.

 

Akizungumza mara baada ya kupokea wanachama hao wapya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed alisema Chama Cha Mapinduzi kimefanya mambo makubwa katika nchi hii ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma kijamii.

 

Aliwataka wanachama hao kuendelea kuunga mkono juhudi za Dk. Samia Suluhu Hassan huku akiwata Mabalozi kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba ili CCM ishinde katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

 

Shemsa pia aliwasisitiza kulipa ada za Uanachama ili waendelee kuwa hai na wanufaike na CCM ikiwemo kugombea nafasi za uongozi huku akisisitiza kuwa CCM imeimarisha mfumo wa utoaji kadi za uanachama ambapo kwa sasa kila mwanachama anapata kadi ya kielektroniki.

 

“Dk. Samia ameelekeza wasaidizi wake tushuke kwa mabalozi na kuwatambua, nanyi ngazi ya wilaya waiteni Mabalozi, shirikianeni nao na tusipange wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu bali tupitishe kiongozi anayekubalika kwa wananchi’’ alisema Shemsa.

 

MWISHO.

 


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akikabidhi kadi za Uanachama kwa wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM) waliojiunga katika kata ya Nyaruhande wilayani Busega.






Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu Lumeni Mathias (aliyeshika kitabu) akisoma kanuni wakati akiwaapisha wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana kata ya Nyaruhande.


Wanachama wapya wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM) kata ya Nyaruhande wilayani Busega.
 

Vijana wa Green Guard wakimvika skafu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika kata ya Nyaruhande wilayani Busega.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akipanda mti kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika jana kata ya Nyaruhande wilayani Busega Mkoani humo.


MNEC wa Mkoa wa Simiyu Gungu Silanga akipanda mti wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika kata ya Nyaruhande wilayani Busega.


Wana CCM wilaya ya Busega wakiwa kwenye maadhimisho ya CCM ya miaka 47 yaliyofanyika kata ya Nyaruhande wilayani humo.





Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم