Gari lenye namba za usajili T T911 BRZ aina ya Prado la Dc TUNDURU, Simon
Chacha baada ya kupata ajali wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Na Samwel Mwanga, Maswa
MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Simon Chacha amenusurika kifo baada ya gari lake binafsi lenye namba za usajili T 911 BRZ aina ya Prado kuacha njia na eneo la jiwe la Hatari kijiji cha Sayusayu wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kwenye Barabara kuu ya Shinyanga-Maswa.
DC Chacha alikuwa akitokea wilayani Sikonge mkoa wa Tabora kwenda Musoma mkoani Mara kupeleka mizigo yake nyumbani kwao hii inatokana na mabadiliko yaliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu kumuhamisha kituo cha kazi na kumpeleka wilaya ya Tunduru.
Ajali hiyo ambayo imetokea leo Machi 19 mwaka huu majira ya saa 4:40 asubuhi kilomita tano kabla ya kufika mjini Maswa na katika gari hilo Dc Chacha alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa pekee yake kwenye gari iliyokuwa imebeba vitu vyake mbalimbali vya nyumbani.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa waliiona gari hiyo ikiwa inayumba na kupoteza mwelekeo na kutoka barabarani na kugonga mawe na kupinduka na mara baada ya ajali hiyo hiyo DC huyo alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Maswa kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge ambaye alifika Hospitali ya wilaya ya Maswa na baadaye kwenye eneo la tukio akiambatana na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo amesema kuwa hali ya Dc Chacha inaendelea vizuri na amepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Amesema kuwa mara baada ya ajali hiyo Dc Chacha alifikishwa katika jengo la wagonjwa wa dharula katika hospitali hiyo na kuanza kupatiwa matibabu na amepata majeraha katika mkono wake wa kulia pamoja na maeneo ya kichwani.
Simiyu Bolg, imefika katika Hospitali ya wilaya ya Maswa na kushuhudia Dc Chacha akiondolewa katika jengo la wagonjwa wa dharula na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa lenye namba za usajili STM 8149 kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
MWISHO
Dc TUNDURU,Simon Chacha akiingizwa kwenye gari la wagonjwa katika
Hospitali ya wilaya ya Maswa ili aweze kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya
Bugando mara baada ya kupata ajali wilayani Maswa Mkoani Simiyu.
Post a Comment