Samira Yusuph Katibu Mtendaji Mpya Klabu waandishi wa Habari Simiyu.





Wanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) Leo wamefanya uchaguzi mdogo wa kumchangua Katibu Mtendaji wa Klabu hiyo ambapo Mwanachama Samira Yusuph amechaguliwa kushika nafasi hiyo.

Samira ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 10 kati ya 15 zilizopigwa, huku nafasi ya Pili ikishikwa na Mwanachama Samwel Mwanga kwa kupata kura tano.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye alikuwa Mwanasheria wa Mkoa huo Mwanahamisi Kawega,  Alisema kuwa hakuna kura iliyoharibika na alimtangaza Samira Yusuph kushinda nafasi hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji Happy Saverine kilichotokea Mwishoni mwa Mwaka Jana.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, Samira amewashukuru wanachama kwa kumchagua, huku akihaidi kutoa ushirikiano na kufanya kazi kwa kujituma ili kuiletea maendeleo klabu na waandishi wa habari kwa ujumla.

MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post