Shemsa ahamasisha WanaCCM kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akiongea na viongozi wa shina, matawi na kata katika Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu Mkoani Simiyu katika ziara ya Tarafa kwa Tarafa.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed amewaagiza viongozi wa matawi, kata na mashina kuhamasisha wanachama kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili wapate sifa za kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

 

Ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa kuimarisha chama na kukagua uhai wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa kanisa Katoliki Mwandoya wilayani Meatu akiwa kwenye ziara ya Tarafa kwa Tarafa.

 

Shemsa amesema ili wana CCM wapate haki ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi wanaowataka lazima wajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura.

 

‘’Tunaelekea kwenye uchaguzi wa wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025, twendeni tukahamashishe wana CCM na wananchi wenye sifa wajiandikishe katika daftari la wapiga kura ili wawe na sifa’’ amesema Shemsa na kuongeza.

 

‘’tujiandikishe ili kukipigia kura Chama Chama Mapinduzi (CCM), ushindi wa vijiji na vitongoji unategemea tutakavyojitokeza kujiandikisha’’.

 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema wanajipanga kupitisha wagombea wanaokubalika, waadilifu na wanaotimiza wajibu wao kwa wanachi.

 

 MWISHO.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akiwa kwenye mkutano wa kuimarisha uhai wa chama katika Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu.


Viongozi wa CCM ngazi ya shina, matawi na kata kutoka Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu wakifuatilia kikao cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani).


Viongozi wa CCM ngazi ya shina, matawi na kata kutoka Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu wakifuatilia kikao cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani).

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed.

 

 

 

 


 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post