Na Costantine Mathias. Maswa.
VYAMA vya Ushirika (Amcos), vimetakiwa kushirikiana na Taasisi za fedha kuwapa elimu wakulima ili waweze kulipwa fedha za pamba kupitia akaunti za benki badala ya kulipwa fedha taslimu.
Hayo yamesemwa juzi na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Maswa, Hezron Ikelesho katika kikao Cha wadau wa pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Halamshauri ya wilaya ya Maswa.
Ikelesho alisema wakulima wakulipwa kwa njia ya benki itaondoa hatari kupoteza au kuibiwa fedha baada ya watu kufahamu kuwa amelipwa fedha za pamba.
"Akaunti za wakulima kwenye mabenki zina masharti nafuu ya kufungua, pia hazina gharama za uendeshaji...mkulima atapata kiasi chote Cha fedha yake na itapunguza hatari ya kuibiwa fedha na atakuwa salama akihitaji kutumia muda wowote" alisema Ikelesho.
Kikao hicho ambacho kilikutana kwa ajili ya kujadili namna sahihi ya ununuzi wa pamba ikiwemo usimamizi wa ubora ambapo walikubaliana wakulima walipwe kwa njia ya fedha taslimu licha ya kutolea angalizo juu ya hatari ya kupoteza fedha za makampuni.
Mwisho.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Maswa, Hezron Ikelesho akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa wakulima wa pamba kulipwa kupitia Taasisi za fedha.
Viongozi wa vyama vya Ushirika (Amcos) wilaya ya Maswa wakiwa kwenye kikao kujadili namna ya kununua zao la pamba.

Post a Comment