Wananchi waililia NEMC kudhibiti Utiririshaji Sumu Dutwa Namba 2.

 Samaki akiwa amekufa kutokana na maji yanayosadikiwa kuwa na sumu yanayotiririshwa kwenye mgodi wa dhahabu Dutwa namba mbili.

 


Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.

 

WANANCHI wa Kijiji na Kata ya Imalamate, wilayani Busega Mkoani Simiyu wameliomba Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuingilia kati na kuidhibiti kampuni ya Kichina inayochimba madini ya dhahabu kwenye mgodi wa Dutwa namba mbili ambao unasadikiwa kutitirisha maji yenye sumu yanayohatarisha maisha ya viumbe hai.

 

Aidha, imedaiwa kuwa maji hayo yenye sumu yameanza kuua samaki na ndege wanaotumika maji yanayotiririshwa kuelekea kwenye mto unaotenganisha kijiji cha Majengo (Bariadi) na Imalamate (Busega) huku mifugo iliyotumia maji hayo ikianza kuzabaa.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Mwenyekiti wa Kijiji cha Imalamate, Paulo Lung’wecha anasema alipigiwa simu na wananchi baada ya kubaini sumu zenye kemikali zinazotiririshwa kutoka mgodini kuelekea kwenye vyanzo vya maji na kuanza kuua viumbe hai wakiwemo ndege na samaki.

 

‘’kuna kipindi kilichopita tulipia yowe na kwenda kwa wawekezaji wetu (wachina), kuna sumu wanatitirisha ambazo zinazoofisha mifugo yetu kwa kunywa maji…eneo letu limethirika kwa sababu ya sumu, samaki waliokuwa wanatumiwa na wananchi kama kitoweo wamekufa, tunaomba wawekezaji watoke katika eneo letu sababu hawawezi kudhibiti sumu zao’’ anasema Lung’wecha.

 

Anaiomba serikali kuingilia kati suala hilo ambalo limeanza kuleta madhara kwa mifugo na viumbe hai wengine huku akihofia wananchi kupata madhara ya kiafya polepole.

 

Magembe Tabu, mfugaji kutoka kijiji cha Imalamate anasema amewakuta ng’ombe wake wakiwa wamezubaa kutokana na kunywa maji yanayosadikiwa kuwa na sumu huku akiiomba serikali kuingilia kati kudhibiti hali hiyo.

 

Juma Kapani anasema licha ya mifugo kuathirika na maji hayo, lakini pia viumbe hai wengine wamekufa, na kwamba baadhi ya wananchi walikuwa wameanza kuokota samaki kwa ajili ya kitoweo.

 

‘’Ng’ombe zangu 60 wameathirika lakini pia kuna viumbe hai wengine wamekufa wakiwemo wadudu, Tumedhibiti baadhi ya wananchi ambao walikuwa wameanza kuokota samaki kwenda kupika…je, haya madhara yatafidiwa kwa namna gani?, binadamu wakipoteza maisha watafidiwa?, kiongozi gani je ili tuweze kufikisha kilio chetu?’’ anahoji Kapani.

 

Diwani wa Kata ya Imalamate Richard Magoti anasema wameshafikisha kilio hicho kwa Uongozi wa wilaya,lakini hawajaona utekelezaji wowote ambapo aliliomba Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kuingilia kati kabla ya wananchi hawajachukua maamuzi magumu.

 

‘’Sehemu ya kwanza tuliyopigia kelele wamerekebisha, lakini sasa kuna sehemu inatiririsha maji na kuja na hii kemikali na kusababisha kuua viumbe hai ikiwemo samaki na kuna wananchi wanalima nyanya na vitunguu na sisi tunatumia hizo mbogamboga…tutaathirika na wananchi watapoteza maisha’’ anasema.

 

Diwani huyo anaiomba serikali kupitia Mamlaka zinavyothibiti uchafuzi wa mazingira kuingilia kati suala hilo ili lisilete madhara makubwa katika jamii, mifugo na vuimbe hai wengine.

 

Akizungumza hivi karibuni, Mwakilishi wa kampuni la wachina la uchimbaji wa madini katika mgodi huo, Wambura Bina amesema watajitahidi kudhibiti hali hiyo ili kulinda mazingira na makazi ya wananchi wanaozunguka mgodi huo.

 

MWISHO.

 

 

Samaki akiwa amekufa kutokana na maji yanayosadikiwa kuwa na sumu yanayotiririshwa kwenye mgodi wa dhahabu Dutwa namba mbili.

 

Maji yanayotiririshwa na Mgodi wa Dhahabu Dutwa namba mbili ambayo yanasaidikiwa kuwa na sumu.


Samaki akiwa amekufa kutokana na maji yanayosadikiwa kuwa na sumu yanayotiririshwa kwenye mgodi wa dhahabu Dutwa namba mbili.


Mboga za majani zinazomwagiliwa maji yanayosadikiwa kuwa na sumu.


Wananchi wa Kijiji cha Imalamate wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiangalia mifugo iliyokunywa maji yanayosadikiwa kuwa na sumu ambayo yanatiririshwa kutoka mgodi wa Dutwa namba mbili unaomilikiwa na Kampini ya Wachina.

 

Wananchi wa Kijiji cha Imalamate wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa eneo lenye maji yanayotiririshwa na Kampuni ya kuchimba madini ya Wachina, yanayosadikiwa kuwa na sumu.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم